habari Mpya


Halmashauri na Wadau Kuisaidia Familia ya Mtoto Anthony.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuri ya Wilaya ya Ngara Bw. Aidan John Bahama, ameitembelea familia ya mtoto Anthony Petro, na kuahidi kwamba kwa kushirikiana na wadau wengine, watamsaidia kumhifadhi karibu na huduma za kijamii.

Bw. Bahama ameyasema hayo akiwa kwenye kijijini Ngudusi kata ya Kabanga, alipoitembelea familia hiyo na kukiri kuwa familia hiyo, inaishi katika mazingira magumu.

Tumempata mfadhili wa kukujenga nyumba, na watoto watapelekwa shule nzuri ili waweze kusoma, Anthony atakwenda wilayani Same mkoani Kilimanjaro kuanza shule, atakaa bweni na atakayemlipia gharama za shule ni mmiliki hiyo.Bw. Bahama alimwambia Baba yake Anthony.
Amesema dada zake Anthony wanatafutiwa shule nyingine, na amewaomba wadau waendelee kujitoa, ili waweze kuisaidia familia hiyo iondokane na mazingira magumu wanamoishi.

Wadau mbalimbali wamejitokeza kuisadia familia hiyo; ambapo baadhi yao wameahidi kujenga nyumba, kuwasomesha watoto pamoja na kuwapatia mahitaji muhimu.
"Mazingira ya familia hii nimeyaona si rafiki nikiwa kiongozi, nitafanya juhudi kuwaondoa katika mazingira haya kwa sababu za kiusalama na hata za kiafya." Amesema Bw. Bahama.

Aidha, Baba yake Anthony Mzee Petro Magogwa amewashukuru wadau wote waliojitokeza kuisaidia familia yake na kuongeza kuwa wakipata elimu itakuwa ndiyo urithi wao.


Habari/Picha Na Shaban Ndyamukama.

Post a Comment

0 Comments