habari Mpya


Wakimbizi Watano Wafa Ajali iliyohusisha magari mawili Ngara, Kagera

Na Samuel Lucas, Amos John,Shabaan Ndyamukama na Auleria Gabriel
Watu watano wamefariki na wengine wengi kujeruhiwa vibaya kufuatia ajali ya magari iliyotokea katika eneo la Kasharazi wilayani Ngara mkoani Kagera 
Muonekano wa mbele basi la  Lugano, kampuni ya Mtipa Investment lilivyoharibika kutokana na ajali
Wananchi wakiendelea kutoa msaada wa kukata miti ili kuliondoa gari
Muonekano wa basi lilivyoanguka


Basi la Adventure likiwafikisha majeruhi katika Hospitali ya Murgwanza wilayani NgaraBaadhi ya wananchi waliofika kushuhudia ajali.
Ajali hiyo imetokea majira ya saa 10 jioni katika mteremko wa mlima k9 ambapo basi moja kati ya nane yaliyokuwa yakipeleka wakimbizi kutoka kambi ya Nduta-Kibondo mkoani Kigoma kuelekea nchini Burundi, kupoteza mfumo wa breki na kuligonga lililokuwa mbele yake na yote kupoteza njia kisha kupinduka


Baadhi ya wahudumu wakiendelea na shughuli za kutoa Huduma kwa majeruhi
Mabasi yote nane yalikuwa yakisafirisha wakimbizi hao kurejea makwao na katika ya waliofariki, wanaume ni watatu na wanawake wawili ambapo wanne walikua abiria mmoja alikuwa mkazi wa Kasharazi aliyekuwa akiendesha baiskeli na ametambulika kwa jina moja la Ndayi


Afisa wa Jeshi la Polisi akikagua kwenye gari kama kuna majeruhi waliobakia
Mmoja wa mashuhuda Bw. Amiri Salum ambaye ni Dereva aliyekuwa nyuma ya mabasi hayo akitokea Biharamulo, amesema wakati magari yakimalizia mteremko ndipo ajali ilipotokea ambapo yote yalielekea kwenye mashamba ya wakulima

Majeruhi wa ajali hiyo wamekimbizwa kwenye hospitali za Murugwanza na Nyamiaga za wilaya ya Ngara kwa ajili ya matibabu

Post a Comment

0 Comments