habari Mpya


RC KAGERA-Pandeni Miti ya Matunda ili Kupunguza Udumavu, Utapiamulo na Kwashakoo hasa kwa Watoto.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera,Mhe. Kijuu akipanda mti wa Mtunda ikiwa ni Kampeini yake ya kupanda miti ya matunda katika Mkoa wa Kagera ili kuondoa tatizo la udaumavu, utapiamulo na kwashakoo kwa wananchi wa Kagera hasa watoto.ametoa wito kwa Taasisi za Serikali na zisizokuwa za Serikali kumuunga mkono katika kampeini ya kupanda miti ya matunda.


Naye Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu akipokea miche ya Matunda na alilishukuru shirika la World Vision Tanzania Kanda ya Kagera kwa kutoa misaada ya mara kwa mara na kushirikiana na Serikali katika shughuli mbalimbali za kuondoa umasikini na kuleta maendeleo kwa wananchi wa Mkoa wa Kagera.
Shirika lisilo kuwa la Serikali World Vision Tanzania Kanda ya Kagera limemuunga Mkono Mkuu wa Mkoa wa Kagera katika Kampeini yake ya kupanda miti ya matunda katika Mkoa wa Kagera ili kuondoa tatizo la udaumavu, utapiamulo na kwashakoo kwa wananchi wa Kagera hasa watoto.

Shirika la World Vision Kanda ya Kagera limeto kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Miche 200 ya miti ya matunda aina mbalimbali yenye thamani ya shilingi milioni 2,000,000/= na Mkuu wa Mkoa wa Kagera aliikabidhi miche hiyo kwa Taasisi za Shule katika Manispaa ya Bukoba ili ikapandwe kwenye mazingira ya Taasisi hizo.
Tayari Mkuu wa Mkoa ameagiza kila mwananchi kupanda miche mitano ya matunda katika eneo lake pia na Taasisi zote zihakikishe zinapanda miche ya matunda katika maeneo yao. World Vision Tanzania Kanda ya Kagera wamekabidhi miche ya matunda 200 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Februari 26, 2018.

Post a Comment

0 Comments