habari Mpya


Rais Magufuli Azindua Jengo jipya la Benki ya CRDB Tawi la Chato Mkoani Geita.


Mmoja wa wacheza ngoma wa kikundi cha Ngoma za asili cha Chato akimwagiwa Rangi kabla ya kuonesha umahiri wake wa kucheza ngoma hiyo.

Burudani hiyo imefanyika leo March 9, 2018 wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifungua wa Tawi jipya la Benki ya CRDB lililopo Chato Mkoani Geita.
Mcheza ngoma za asili wa kikundi kutoka Chato akionesha umahiri wake wa kucheza ngoma katika sherehe za ufunguzi wa Tawi la Benki ya CRDB lililopo Chato Mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia wakati kikundi cha ngoma za asili kutoka Chato(hakionekani pichani) kilipokuwa kikitumbuiza katika viwanja wa Tawi la Benki ya CRDB kabla ya ufunguzi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia kwa kupiga makofi pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB Ally Laay pamoja na Naibu Waziri wa Fedha Dkt. Ashatu Kijaji wakati msanii wa kikundi cha ngoma za asili cha Chato alipokuwa akitoa burudani ya ngoma hiyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipiga ngoma wakati msanii wa Msechu Bendi Peter Msechu alipokuwa akiimba mara baada ya kufungua tawi hilo la Benki.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB Ally Laay, Naibu Waziri wa Fedha Dkt. Ashatu Kijaji pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei kabla ya ufunguzi wa tawi hilo.

PICHA NA IKULU.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mhe Dkt. Magufuli amesema kuwa uwepo wa Benki hiyo utarahisisha huduma za uhifadhi fedha kwa wafanyabiashara wa samaki Wilayani Chato sambamba na wananchi ambao kwa kiasi kikubwa katika msimu wa Kilimo wamenilima Pamba kwa wingi.

Ameipongeza Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kwa kuzifungia baadhi ya Benki nchini na kuzipa onyo zingine ambazo zilikuwa zinafanya kazi kwa mazoea na kwenda kinyume na utaratibu wa sheria za uendeshaji.

Rais Magufuli ameiomba benki ya CRDB kupunguza riba ya mikopo kwani ni asilimia 16 pekee ya watanzania ndio wanaohudumiwa kwenye Benki nchini hivyo ili wananchi wote waweze kukopa na kuweka mitaji yao midogo kwa ajili ya faida yao ya Sasa na badae ni lazima kuwa na riba rafiki kwa wananchi.

Katika hatua nyingine Rais Magufuli amewahamasisha wananchi kutunza fedha zao benki na kuachana na dhana ya kuhifadhi fedha majumbani jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa fedha hizo na maisha yao wenyewe.

Aidha, Mhe Rais Magufuli alikataa ombi la Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Tanzania Dkt Charles Kimei aliyetaka Benki hiyo kuitwa CRDB JOHN POMBE MAGUFULI-CHATO huku akisema kuwa isalie kuitwa CRDB tawi ka CHATO.

Dhifa ya uzinduzi wa Benki hiyo ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri Wa Nishati Mhe Medard M.Kalemani (Mb), Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Mb), Mkuu Wa Mkoa Wa Geita Mhandisi Robert Gabriel, Naibu Waziri Wa fedha na Mipango Dkt Ashatu Kijazi (Mb), Naibu Gavana Wa Benki Kuu Tanzania Dkt Bernard Yohana Kibese, Balozi Wa Denmark nchini Tanzania Mhe Einar Hebogard Jensen, Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi CRDB Tanzania Ndg Martin Mmari, Mkurugenzi Mtendaji CRDB Tanzania Dkt Charles Kimei, na Wabunge wa majimbo mbalimbali ikiwemo jimbo la Busanda na Mbogwe.

Post a Comment

0 Comments