habari Mpya


Radio Kwizera yaja na Kampeni ya Usafi wa Mazingira.

Mkurugenzi wa Radio Kiwzera Padre Damas Missanga SJ  ( kulia pichani ) akishiriki zoezi la usafi wa Mazingira March Mosi,2018 katika Mtaa wa Barabara ya Ngara- Jankisheni katikati ya Mji wa Ngara,mkoani Kagera wakati wa zoezi la usafi wa Mazingira unaoratibiwa na Kituo hicho cha Radio katika Mji wa Ngara ikiwa ni Kampeni iliyoanzishwa Kuwakumbusha Viongozi na Wananchi wilayani humo ikiwa ninamna mojawapo ya kuhakikisha mji huo unakuwa safi wakati wote.

Kituo cha Radio Kwizera cha wilayani Ngara mkoani Kagera kimeanzisha kampeni ya kuwakumbusha Viongozi na Wananchi wilayani humo kudhibiti watu wanaochafua mazingira kwa kutupa taka ovyo ikiwa ninamna mojawapo ya kuhakikisha mji huo unakuwa safi wakati wote.
Akizungumza wakati wa zoezi la usafi March Mosi,2018, Mkurugenzi wa Radio Kwizera FM Padre.Damas Missanga SJ, Aliwashauri wakazi wa Ngara na wageni kujiepusha na utupaji wa taka ovyo, na kwamba suala la usafi ni la kila mtu na kwamba kwenye kampeni ya usafi wao Wanaihamasisha Jamii,Viongozi mbalimbali na Mamlaka za Usafi wilayani Ngara kutimiza wajibu wao katika kushiriki kwenye zoezi la usafi wa mazingira mara kwa mara katika maeneo yao ili kuepukana na magonjwa yatokanayo na uchafu kama vile kuhara na kipindupindu.
Uchunguzi wa Radio Kwizera FM umebaini kwamba, katika maeneo ya Mji wa Ngara,  mwitikio wa wananchi katika suala la usafi ni mdogo mno huku wengi wao ameeleza kwamba, changamoto kubwa ni uchafu wa kudumu kwenye maeneo ya Vizimba vya kutupia taka maeneo ambayo usafi wa mazingira haufanyiki kama inavyotakiwa.

Kumbukumbu zinaonyesha kwamba, katika kuhakikisha kampeni ya usafi wa mazingira kuwa ni ya kitaifa na endelevu, mwaka 2015 na 2016 Rais Magufuli alilazimika kufuta baadhi ya sherehe za kitaifa na kuzifanya kuwa siku za usafi kitaifa pamoja na kuelekeza fedha kwenye upanuzi wa miundombinu.

Post a Comment

0 Comments