habari Mpya


Radi Yajeruhi Walimu wawili na Wanafunzi 63 Mkoani Kagera.

Wanafunzi waliojeruhiwa wakipatiwa Huduma ya kwanza.

Kufuatia Mvua zinazoendelea Kunyesha Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera, zimesababisha radi  iliyojeruhi Walimu wawili na Wanafunzi 63 katika Shule ya Msingi Kyakailabwa.

Mwalimu Mkuu wa hiyo,Mwl. Jovina James Rugaimukamu, ameieleza kuwa tukio hilo limetokea asubuhi ya March 22,2018, ambapo pamoja na kujeruhi watu hao, pia limeharibu miundombinu ya shule hiyo, na kuleta hofu wakati huu wa mvua kwasababu ya uhaba wa mitego ya radi katika shule hiyo.
Baadhi ya wazazi wamesema kuwa wamepokea taarifa za radi hiyo kwa mstuko mkubwa, kwasababu idadi ya watoto hao zaidi ya 60 waliojeruhiwa sambamba na walimu wao wawili wa kike siyo la kawaida, na kwamba baadhi ya watoto walioruhusiwa kurudi nyumbani hawako kwenye hali ya kawaida, wengine wakitembea kwa kuchechemea ilhali wengine wakiwa na hofu ya kutokea tena tukio kama hilo.
Katibu wa hospitali ya mkoa wa Kagera Kilwanila Kiiza, amethibitisha kuwapokea  majeruhi kadhaa saa tatu asubuhi, ambapo kati ya hao wawili walikuwa wamepoteza fahamu, na kati ya 7 waliolazwa wawili ni wawilimu na watoto watano.

Amesema kuwa wamejitahidi kuwapa huduma ya mazoezi ya kupunguza mionzi miilini, na wataendelea na uangalizi wa karibu kwa saa 24, akiwataja walimu kuwa ni Mwl.Witnes Kabyemela na mwl.Theodata Prosper, na kwamba wanafunzi waliolazwa ni wa darasa la pili hadi la saba.

Post a Comment

0 Comments