habari Mpya


Picha: Misa ya Mazishi ya Padre Mutabazi mjini Rulenge.

Askofu wa Jimbo la Rulenge-Ngara Muhashamu Severine Niwemgizi  akiwaongoza Mamia ya waumimi wakatoliki na wasio wakatoliki  wakati wa ibada ya mazishi ya aliyekuwa Paroko msaidizi wa Parokia ya Chato Jimbo Katoliki la Rulenge-Ngara Padre Mosinyori Emmanuel Mutabazi yaliyofanyika March 27,2018 katika makabuli ya Mapadre mjini Rulenge wilayani Ngara mkoani Kagera.

 Hawa Masista ni Ndugu wa Marehemu Mosinyori Emmanuel Mutabazi waliposhiriki kuweka shada la maua wakati wa mazishi yake yaliyofanyika Juzi March 27,2018 katika makabuli ya Mapadre mjini Rulenge wilayani Ngara mkoani Kagera.
Akitoa Mahubiri katika ibada hiyo ya mazishi iliyofanyika katika Kanisa Katoliki mjini Rulenge, Askofu wa Jimbo la Rulenge-Ngara Muhashamu Severine Niwemugizi amesema Jimbo hilo limepata pigo la kuondokewa na Padre Mosinyori Mutabazi kwani jimbo lilikuwa likimtegemea kama mtafsiri wa biblia

Askofu Niwemugizi amesema Padre Mosinyori Emmanuel Mutabazi katika kipindi chote cha miaka 48 ya utume wake amekuwa akifanya kazi kwa bidii huku akiwaheshimu wakubwa na wadogo.
 

Kwa upande wao waumini waliojitokeza kuuga mwili wa mosinyori Mutabazi wamesema wamempoteza mtu muhimu sana katika kanisa kutokana na wataendelea kumuenzi na kumuombea kwa yote mema ambayo aliyafanya kwa maendeleo ya kiroho.

Padre Mosinyori  Emmanuel Mtabazi alikuwa mtaalam wa kutafsiri biblia takatifu na Paroko msaidizi wa Parokia ya Chato mkoani Geita ambaye alifariki alfajiri ya Marchi 25,2018.

Padre Mosinyori Emmanuel Mtabazi enzi za uhai wake amewahi kuwa mkufunzi katika chuo kikuu cha Kweya Nairobi nchini Kenya na amekuwa katika utume wake kwa kipindi cha miaka 48.

Post a Comment

0 Comments