habari Mpya


Muonekano wa Jengo la Upasuaji Vituo vya Afya Murusagamba na Mabawe.

MURSAGAMBA%2B2
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Ngara Mhe.Erick Nkilamachumu akiwa na Viongozi mbalimbali wakati walipotembelea Jengo linalojengwa Kituo cha Afya Murusagamba.

 Halmashauri ya wilaya ya Ngara mkoani Kagera imepokea Sh800 milioni kutoka wizara ya afya Maendeleo ya jamii, jinsia wazee na watoto zitakazotumika kuboresha  miundombinu ya kutolea huduma za afya katika halmashauri hiyo.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara Mhe.Erick Nkilamachumu alibainisha hayo March 24, 2018 alipofanya ziara ya kukagua Ujenzi na Uboreshaji wa Miundombinu katika vituo vya afya Mabawe na Murusagamba wilayani humo.

Mhe.Nkilamachumu alisema kati ya fedha hizo Sh 400 milioni zitatumika  kituo Afya Mabawe  na nyingine Kituo cha Murusagamba kwa kujenga majengo ya Upasuaji, Kulaza Wagonjwa,Ujenzi wa nyumba za Watumishi na Miundombinu mingineyo.
MURSAGAMBA%2B3
Jengo la Afya Kituo cha Afya Murusagamba.
 
Naye Kaimu Mganga mkuu wa wilaya ya Ngara Dkt Godian Beyanga alisema upanuzi wa kituo cha Afya Murusagamba   kinakadiriwa kuhudumia watu 36,060 katika vijiji tisa na vitongoji 53   kata za Murusagamba, Muganza na Nyamagoma na kitasaidia wananchi wanaotumia gharama kubwa hadi Hospitali ya wilaya hiyo.
 
 Upanuzi wa kituo hiki bado unahitaji umeme wa uhakika kihuduma maana unaotumika ni wakutegemea jua jambo ambalo ni hatari wakati wa mvua kufanya upasuaji kwa wanawake wajawazito wanaojifungua” Alisema Dkt Beyanga.
 
Hata hivyo Afisa Mipango wa Halmashauri hiyo Bw.Ghalib Mkumbwa alisema   kituo cha Afya cha kata ya Bukiriro  kinachotegemewa  na kata saba kinasubiria fedha toka Serikalini kupanua majengo yake   kuhudumia   wananchi kwa sekta ya Afya
 MURSAGAMBA%2B4

MABAWE%2B1

MABAWE%2B2
Mazungumzo na Watumishi wa Kituo cha Afya Mabawe.
 
Akiwa kituo cha Afya Mabawe, Mhe.Nkilamachumu aliwataka wajumbe wa kamati ya ujenzi kuacha malumbano ya kusimamia majengo yaliyoanzishwa,bali wafanye     vikao vya maamuzi na kushirikisha wananchi kusogeza vifaa vinavyohitajika.
 
Kituo cha Afya Mabawe kinahudumia wakazi 15,654 kutoka vijiji vitano vya kata ya Mabawe  na vingine vya kata ya  Kabanga, Kanazi na Mugoma ambapo wananchi hufika kupewa huduma za matibabu kwa maradhi ya aina mbalimbali.
 
Aidha aliwashauri wananchi kuchangia bima ya Afya kupitia CHF Sh15,000 kila kaya na kutibiwa watu sita mwaka mzima, na kuagiza uongozi wa kituo hicho kupunguza gharama za kulaza wagonjwa kutoka Sh10,000 kwa siku hadi Sh2,000.
MABAWE%2B3

MABAWE%2B4

MABAWE
Jengo katika kituo cha afya Mabawe..Picha/Habari  Na Shaaban Ndyamukama.

Post a Comment

0 Comments