habari Mpya


Muonekano wa eneo la Kituo cha Ushuru cha Pamoja (OSBP) cha Kabanga wilayani Ngara mkoani Kagera.

Huu ni muonekano wa eneo la Kituo cha Ushuru cha Pamoja (OSBP) cha Kabanga wilayani Ngara mkoani Kagera ambapo kituo hicho kilichoko eneo la Kabanga nchini na Kobero nchini Burundi, kitasaidia uvukaji wa abiria na usafirishaji wa bidhaa.

Picha hizi zilipigwa Jana March 16,2018 wakati hali ya hewa ikiwa ya ukungu na mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali wilayani Ngara.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Serikali ya Tanzania katika Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, matumizi ya vituo hivyo vya pamoja, yatafanya msafiri kukaguliwa sehemu moja ya anakoelekea, huku idara zote zikiwa katika jengo moja.

vVituo hivyo vya pamoja, vitadhibiti na kuboresha utoaji huduma za kiforodha na uhamiaji kwa ushirikiano na ufanisi zaidi, hivyo kukuza biashara, uwekezaji, uzalishaji na usafirishaji.
 


Post a Comment

0 Comments