habari Mpya


Mtoto Anthony Petro (10) Kusaidiwa.

29258699_1796653880374514_4180979035762851840_o
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara Aidan Bahama amesema mtoto Anthony Petro (10) amepata mfadhili wa kumsomesha kutoka  Same mkoani Kilimanjaro na wadogo zake watasomeshwa na halmashauri ya wilaya ikisaidiana na wafadhili watakaojitokeza.
 
 Bahama alisema  kwamba mfadhili huyo ni Isihaka Msuya aliyejitolea kumwendeleza mtoto Anthony hadi Mwenyezi Mungu atakapomfikisha na atampatia mahitaji muhimu ya haki za binadamu.
 
Alisema idara ya ustawi wa jamii wilayani Ngara kwa kushirikisha kiongozi wa kiroho wa kanisa katoliki parokia ya Ntungamo Padre Pamphilius Kitondo, wamefungua akaunt benki ya CRDB  namba 0152346697000 ili wenye moyo wa kuchangia wajitokeze kupitia akaunti hiyo.
 
"Tunafanya juhudi ya kupata shule ya kuwapeleka shule  dada zake Anthony kuweza kusoma wakiwa bwenini na kupata mahitaji muhimu ikiwemo chakula na kuimarisha afya zao na halmashauri itahusika" Alisema Bahama.

29260999_1796654460374456_8067031600841359360_o
Afisa Ustawi wa Jamii wilayani Ngara Musa Niyonsaba Balagondoza akiwa nyumbani kwa Babake na Anthony.
29257734_1796654497041119_148138915302211584_o
Mwanafunzi huyo Anthony Petro pichani kulia, wiki iliyopita alijulikana kupitia mitandao ya kijamii na vyombo mbalimbali vya habari ambapo anaishi maisha kuombaomba  wasamaria wema baada ya baba yake Petro Magogwa kutokuwa na uwezo kiuchumi wa kupata chakula cha familia.
 
Alisema maisha yake ni ya shida kwa familia kukosa mto wa mchana akishindia andazi moja na maji baada ya baba yao kukosa chakula na kutokuwa na uwezo kifedha wakati mwingine yeye na wadogo zake hutumia maparachichi kama mlo wa mchana au usiku.
 
Mazingira ya mwanafunzi huyo  sio ya usalama kwani familia inaishi mbali na kijiji mpakani na nchi jirani ya Burundi nyumba yao iliyobomoka imezungukwa na msitu  kwa maana ya miti ya parachichi, mifenezi na karatusi huku kwa majirani kukiwa na miti ya karibea na migrevelia.
 
Tuhamishwe eneo hili na kujengewa sehemu nyingine, hapa watu wabaya wanaweza kuja na kutuua au kutuibia ila namshukuru Mungu nikishiba nikaenda shule nataka niwe mwalimi nakufundisha  wengine”Alisema Anthony.
 29244672_1796654377041131_3136486059307696128_o

29313650_1796654330374469_80759811959947264_o
Afisa Ustawi wa Jamii wilayani Ngara Musa Niyonsaba Balagondoza alipoutembelea Uongozi wa Shule anayosoma Anthony.

29261777_1796653923707843_3550775035562033152_o
Pia alisema akipata chakula na kushiba hatakuwa na mawazo ya kwenda kuomba omba mpakani mwa nchi ya Burundi eneo la  Kobero na kabanga mjini hivyo, atahuduria masomo na kuhakikisha anafuata atakachoelekezwa na walimu hatimaye atimize malengo  kimaisha. 
 
Afisa Ustawi wa Jamii wilayani Ngara Musa Niyonsaba Balagondoza,  ametembelea Shule ya msingi Ngundusi kubaini mahudhurio ya Mwanafunzi Anthony na kufika kwa baba yake na kusema serikali na jamii wakiungana mtoto huyo na ndugu zake wataboreshewa maisha.
 
Amesema idara yake inasimamia na kulinda haki za watoto kwa mujibu wa sheria namba 21 ya mwaka 2009, hivyo anawashukuru wananchi walioibua mtoto huyo kwa kutumia mitandao ya kijamii ambapo baadhi ya watu walioguswa wameanza kujitokeza kusaidia.
Ngara, Na Shaaban Ndyamukama.

Post a Comment

0 Comments