habari Mpya


Milioni 69.56 zawafikisha Viongozi 15 wa Chama cha Ngara Farmers Mahakamani.

Taswira ya Mji wa Ngara 

Viongozi 15 wakiwemo watendaji wa chama cha Ngara Farmers wilayani Ngara mkoani Kagera, wamefikishwa katika mahakama ya wilaya hiyo kwa tuhuma za kuhujumu fedha za Chama shilingi milioni 69.56 na kushindwa kutimiza malengo ya wanachama.

 Mbele ya hakimu wa mahakama ya wilaya ya Ngara Andrew Kabuka, mwendesha mashtaka wa jeshi la polisi Jumanne Maatu, amewataja wiongozi hao kuwa ni Thomson Seyongwe, Paschal Kageze, John Shimilimana, Allan Mnanka, Johas Rugwiza, Joyce Rutebuka na Pascal Minani.  

Wengine kuwa ni Bazikus Thadeo, Jacob Miburo, Beltila Silvan, Ruben Ruvugo, Marton Rugegwa, Siliacus Rusaku, Steven Runzanga na Sostenes Deogratias ambao wote  wanatuhumiwa kukihujumu chama cha Ngara Farmers kati ya mwaka 2012 hadi 2014.

Watuhumiwa hao kwa pamoja wamekana mashtaka yanayowakabili ambapo kesi yao imeahirishwa na itasikilizwa tena mahakamani hapo Machi 23 mwaka huu,2018 

Post a Comment

0 Comments