habari Mpya


Jeshi la Polisi latoa Mwezi mmoja kwa Wakimbizi Kigoma kusalimisha Silaha.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kigoma ACP Martin Othieno ametoa muda huo March 21, 2018 kufuatia kuongezeka kwa matukio ya uhalifu yanayodaiwa kufanywa na wakimbizi kutoka nchini Burundi ambao wanamiliki silaha kinyume cha sheria.

Jeshi la Polisi mkoani Kigoma limetoa mwezi mmoja kwa raia wa Burundi waishio katika kambi za Wakimbizi mkoani humo kusalimisha silaha kabla ya kufanyika kwa msako mkubwa baada ya kubainika wengi wao kumiliki silaha hizo kinyume cha sheria. 

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kigoma ACP Martin Othieno ametoa muda huo leo kufuatia kuongezeka kwa matukio ya uhalifu yanayodaiwa kufanywa na wakimbizi kutoka nchini Burundi ambao wanamiliki silaha kinyume cha sheria.

Akizungumzia tukio la hivi karibuni Kamanda Othieno amesema polisi bado inawasaka watu watatu kati ya watano wanaodaiwa kuwa majambazi kufuatia kutoroka baada ya majibishano ya risasi katika eneo la pori la Makere Wilayani Kasulu ambapo majambazi wawili walifariki papo hapo.

ACP Othieno amewataja waliokufa kuwa ni washirika wawili, raia wa Tanzania mkazi wa Kasulu Nobert Andrew na Raia wa Burundi Bukuru Steven mkazi wa kambi ya Nyarugusu waliokuwa wakimiliki bundiki AK47 na risasi 41.

Post a Comment

0 Comments