habari Mpya


Idara ya Maji Ngara yabanwa Kuhusu Matumizi ya Milioni 24 za Mradi wa Maji.

IMG_20180302_121610
Aliyesimama ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara mkoani Kagera na Diwani wa kata ya Bukirilo Bw.Erick Emmily Nkilamachum,kulia kwake ni Makamu wake Bi.Giogina Mnyonyela na Mkuu wa wilaya Bw.Michael Mtenjele.

IMG_20180302_122450
Diwani wa kata ya Ntobeye,Bw.John Ruzige ambaye pia ni Mjumbe Kamati ya fedha na Mipango.
 
Idara ya Maji wilayani Ngara mkoani Kagera imetakiwa kutoa maelezo ya kina juu ya fedha ya mradi wa maji wa K9 ambayo ni milioni 24 kati 78 zilizo kuwa zimtoleo katika kutekeleza mradi wa maji K9 ambapo fedha hiyo ilihamishiwa Ngara mjini.
 
Agizo hilo limetolewa na Bw.John Ruzinge, Diwani wa Kata ya Ntobeye wilayani Ngara wakati wa kikao cha kamati ya ushauri kilicho fanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo hivi karibuni.
 
Nikuombe Mhadisi wa maji Bi. Godliver ifikapo mach 15 mwaka huu katika kikao cha baraza la madiwani uje na majibu ya kina utuambie ulitumia kigezo gani kuhamisha fedha za mradi wa maji wa k9 na kuzielekeza fedha hizo katika sehem nyingine bila kupata lidhaa katika kikao cha kamati ya mipango na fadha” alisema Ruzige.
 
Aidha, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Bw.Erick Emmily Nkilamachum amesikitishwa na kitendo cha Mhandisi wa maji kuchukua maamuzi ya kubadilisha matumizi ya fedha katika eneo la mradi nakudai kuwa huenda hizo zilikuwa njia za kutaka kuhujumu pesa hiyo.
 
Mh. Mwenyekiti mimi niseme tu pesa hizi zilitaka kupigwa haiwezekani mhandisi pekeyake anachukua milioni 24 zilizopo katika mradi wa maji k9 zaidi ya milioni 100 bili kushirikisha kikao cha baraza la madiwani anajichukulia maamuzi mwenyewe tu mimi ni Mwenyekiti wa baraza la mabiwani na baraza zima la madiwani hawajui nawasiwasi pesa hizo zilitaka kupigwa kabisa ” alisema Nkilamachum.
 
  IMG_20180302_121413
  Aliyesimama ni Mbunge wa Jimbo la Ngara mkoani Kagera Bw.Alex Rafael Gashaza.
 
Sakata hilo liliibuliwa na Mbunge wa Jimbo hilo Bw. Alex Rafael Gashaza kuhoji kuwa pesa zaidi  ya shilingi milioni 100 zilizoletwa katika mradi wa maji K9 zimefanya nini mpaka sasa mbona bado Wananchi wa K9 wanaendelea kupata shida ya maji.
IMG_20180302_121540
Mhandisi wa maji wilayani Ngara mkoani Kagera Bi.Godliver J.Gwambasa akitoa utetezi wake.
 
Katika utetezi wake mhandisi wa maji Bi.Godliver Gwambasa amesema kuwa waliamua kutoa milioni 24 kuzipeleka Ngara mjini katika shughuli za miradi ya maendeleo ya maji kwa kuwa waliona kuwa hizo milioni 78 zilizo baki zinaweza kutosheleza mradi wa maji k9.
 
Mh.Mwenekiti tuliamua kuchukua MILIONI 24 kuzileta kusadia katika miradi ya maji Ngara mjini kwakuwa tuliona kuwa kiasi kilicho bakia cha shilingi milioni 78 kinatosheleza kukamilisha mradi wa maji k9” alisema Godliver.
IMG_20180302_124143
Afisa Mipango Bw Ghalibu  Mkumbwa akiwasilisha taarifa ya makisio ya bajeti kwa mwaka 2018/2019 katika kikao hicho cha kamati ya ushauri.
 
Naye  Afisa Mipango Bw Ghalibu  Mkumbwa amesema kuwa kosa ambalo wamelifanya ni kutopeleka mabadiliko katika vikao lakini walifanya mabadiliko hayo kwa kuyapeleka mamlaka ya maji Ngara mjini  baada ya mradi wa K9 kupatiwa shilingi  milioni 78.
IMG_20180302_120549
Pichani aliye simama ni mkuu wa wilaya ya Ngara mkoani Kagera Luteni Kanali Michael Mtenjele wakati wa ufunguzi wa kikao cha kamati ya ushauri wilaya ambapo kimsingi katika kikao hicho yeye ndio Mwenyekiti.
IMG_20180302_132920
Wakwanza kutoka kulia ni mkuu wa wilaya  ya Ngara mkoani Kagera Luteni Kanali Michael Mtenjele walipi aliye simama ni katibu tawala wa wilaya hiyo Bw.Vedastus Tibaijuka na anaye fuata ni Mbunge wa Jimbo la Ngara Bw.Alex Rafael Gashaza.

Post a Comment

0 Comments