habari Mpya


Damu Yako,Maisha Yangu -Ungana na Radio Kwizera FM Kuchangia Damu Salama.

Wanafunzi wa Shule ya Nyanshenye iliyoko Kata Kahororo Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera wakishiriki kuchangia Damu  wakati wa zoezi hilo lililoongozwa na Kamati ya Damu Salama mkoa wa Kagera.

Mtalamu kutoka Kamati ya Damu Salama mkoani Kagera akimpima Wanafunzi wa Shule ya Nyanshenye iliyoko Kata Kahororo Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera kujua afya yake kabla ya zoezi la kuchangia Damu.

Wanafunzi wa Shule ya Nyanshenye iliyoko Kata Kahororo Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera wakijianda kushiriki zoezi la kuchangia Damu lililoongozwa na Kamati ya Damu Salama mkoa wa Kagera.
Zoezi hilo limezifikia Taasisi mbalimbali zilizopo katika Manispaa ya Bukoba na Chupa ( Unit )  75 za damu zimekusanywa.

Zoezi hilo limekuwa likitembelea taasisi mbalimbali zikiwemo Shule,Vyuo, Taasisi za Kidini, Redio Kwizera pia imepongezwa kwa Kampeini yake ya kuchangia Damu kupitia kipindi cha Asubuhi Jema.
 


Post a Comment

0 Comments