habari Mpya


Ajichoma Moto Ndani ya nyumba baada ya Kumuua Mama Mkwe.

IMG_1467
Kijana anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 32 mkazi wa kitongoji cha Nyakahanga kata ya Rusumo Wilayani Ngara Mkoani Kagera amejiua kwa kujichoma moto ndani ya nyumba baada ya kumuua Mama Mkwe wake pamoja na kumjeruhi Mke wake sehemu mbalimbali za mwili kwa kumchoma na kisu.
 
Tukio hilo limetokea majira ya saa 5 usiku wa kumkia leo March 17,2018 ambapo Bw Joseph Medadi amemuua Mama Mkwe wake Bi Elizabeth Simoth anaeyekadiriwa kuwa na umri wa miaka 70 na kisha kumjeruhi mke wake Elice Joseph anaekadiriwa kuwa na umri wa miaka 28 ambaye amelazwa katika hospitali ya Murugwanza wilayani Ngara.
 IMG_1468

IMG_1471
Mwili wa Marehemu eneo la tukio.
 
Akizungumzia tukio hilo, Mwenyekiti wa kijiji cha Rusumo Bw Dauson Kadende amesema baada ya Bw Joseph Medadi kutekeleza tukio hilo ndipo akachukua uamuzi wa kujichoma moto ndani ya nyumba kwa kutumia petroli hali iliyosababisha kifo chake.
  IMG_1479

IMG_1481

IMG_1483
Nyumba ya Mama Mkwe ilivyoteketea kwa moto.
 
Kwa upande wake msemaji wa familia hiyo Bw Ezeckia Simion amesema chanzo cha tukio hilo ni kuwepo kwa  mgogoro wa kifamilia baina ya Marehemu Bw Joseph na Mke wake.
 IMG_1489

IMG_1495
Juu na Chini Pichani ni Baadhi ya wakazi wa Nyakahanga kata ya Rusumo Wilayani Ngara Mkoani Kagera wakiwa eneo la tukio kufatilia na kufanya taratibu zinginezo.
 
Mkuu wa Jeshi la Polisi Wilayani Ngara Bw Abeid Maige amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba upelelezi juu ya tukio hilo bado unaendelea.
 IMG_1496
IMG_1465
Muonekano wa nyumba ilivyoungua ndani eneo la tukio.

Post a Comment

0 Comments