habari Mpya


Ajali ya Wakimbizi Ngara: Idadi ya Vifo yaongezeka


Na Samwel Lucas, Shabaan Ndyamukama
Idadi ya vifo vya wakimbizi waliopata ajali kwenye mteremko wa K9 katika kijiji Kasharazi wilayani Ngara mkoani Kagera imeongezeka na kufikia nane baada ya wawili kufariki wakipatiwa matibabu katika Hospitali ya Murugwanza na mmoja katika hospitali ya Nyamiaga


Mkuu wa Wilaya ya Ngara Luteni Kanali Michael Mtenjele akitazama majeruhi katika Hospitali ya Murgwanza wilayani Ngara

Afisa mwandamizi wa Shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR wilayani Ngara Bi. Irene Babu amesema kati ya hao nane waliopoteza maisha, sita ni wakimbizi na watanzania ni wawili ambapo kati ya hao watanzania, mmoja alikuwa mwendesha baiskeli na mwingine alikuwa mfanyakazi wa shirika la Afya la kuhudumia wakimbizi (IOM)


Afisa mwandamizi wa Shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR wilayani Ngara Bi. Irene Babu
 

 Mganga mkuu wa Hospitali ya Murugwanza Dr. Remmy Andrew amesema katika hospitali hiyo alipokea majeruhi 65 kati yao 30 ni wanawake na 35 na kwamba waliotibiwa na kuruhusiwa ni 40 na wanaohitaji rufaa kwenda hospitali ya Bugando saba

Mkuu wa wilaya ya Ngara Luteni Kanali Michael Mtenjele akipokea taarifa kutoka kwa mganga Mkuu wa hospitali ya Murgwanza

Naye mganga mfawidhi wa hospitali ya Nyamiaga Dr. Simon Kyamwenge amesema hospitali hiyo ilipokea majeruhi 31 kati yao wanaume ni 24 na wanawake 7 na kwamba mpaka sasa ameruhusiwa mtu mmoja pekee

 Pia Dr. Kyamwenge amesema majeruhi 12 wenye hali mbaya wamepewa rufaa ya kupelekwa katika hospitali ya Bugando jijini MwanzaMkuu wa Wilaya ya Ngara Luteni Kanali Michael Mtenjele akiwajulia hali majeruhi wodini

Mkuu wa Wilaya ya Ngara Luteni Kanali Michael Mtenjele amesema pamekuwa pakitokea ajali katika eneo la K9 kutokana na baadhi ya madereva kutokuwa makini kwani ni sehemu yenye mteremko mkali hivyo kila dereva anayetumia barabara hiyo anapaswa kuwa muangalifu


Mikakati ya kuwasafirisha majeruhi kwenda Hospitali ya rufaa Bugando Mwanza

Mpaka sasa majeruhi 12 tayari wamekwishasafirishwa kwa ndege ya UNHCR kwenda hospitali ya Bugando kupitia uwanja wa ndege wa Ruganzo uliopo wilayani Ngara
Uwanja wa ndege Ruganzo Ngara
 


 

Baadhi ya wagonjwa wakiandaliwa kwa safari ya  Bugando Mwanza

 
Post a Comment

0 Comments