habari Mpya


Real Madrid na Liverpool zatakata Mechi Kombe la Mabingwa Barani Ulaya.

Real Madrid imeishushia kipigo cha bao 3-1 timu ya Paris Saint German – PSG katika Mechi ya Kombe la Mabingwa Barani Ulaya iliyopigwa pale Santiago Bernabeu, Hispania.

PSG ndiyo walikuwa wa kwanza kupachika goli kupitis kwa Rabiot dakika ya 33 ambapo dakika ya 45 Ronaldo aliisawadhishia Madrid kabla ya kwenda mapumziko.

Ronaldo alitupia bao la pili na la kuongoza kwa Madrid dakika ya 83, ambapo sasa ameweka rekodi ya kufunga mabao 101 katika mechi 95 za Uefa Champions League alizocheza akiwa na Madrid huku Marcelo alifunga ukurasa wa mabao kwa Madrid kunako dakika ya 86 na kufanya mchezo umalizike kwa 3-1, PSG wakitepeta mbele ya Madrid.
Nao Timu ya Liverpool ya Uingereza imeishushia kipigo cha mbwa mwizi timu ya Porto baada ya kuinyuka bao 5-0 mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya huku Sergio Monwy akitupia hat trick.

Post a Comment

0 Comments