habari Mpya


Ngara Mshindi wa Pili Bonanza la Michezo ya Jambo Bukoba mkoani Kagera.

Kikombe cha Mshindi wa Pili Jambo Bukoba.

Matokeo ya Bonanza la michezo mbalimbali inayoandaliwa na Shirika la Jambo Bukoba la mkoani Kagera kwa Mabingwa wa Wilaya Nane wa Shule za Msingi limefanyika Jana January 26/2018 katika uwanja wa Gymkhana mjini Bukoba na Halmashauri ya Bukoba imeibuka Bingwa wa Mkoa wa Jambo Bukoba kwa kupata Alama 92 huku mshindi wa Pili akiwa ni Halmashauri ya wilaya ya Ngara iliyowakilishwa na Shule ya Msingi Ngoma kwa kuibuka na Alama 90.


Pamoja na kushirikisha Shule Nane za Halmashauri zote Nane za Mkoani Kagera,Mshindi pamoja na mambo mengine atapata ufadhili wa kuboreshewa miundombinu katika shule yake.
Wachezaji Kutoka Shule ya Msingi Ngoma/Halmashauri ya wilaya ya Ngara.

Jambo Bukoba ni Shirika lisilokuwa la Serikali linalofanya kazi mkoani Kagera kwa kushirikiana na serikali ya Mkoa. 

 Jambo Bukoba ilianzishwa Mkoani Kagera kwa kusaidia watoto hasa Wanafunzi wa Shule za Msingi kuanzia miaka 5 hadi 19 kujenga Afya zao Kimichezo ili kujikinga na Maabukizi ya UKIMWI, kuweka haki sawa katika Elimu kupitia michezo kwa Wasichana na Wavulana. 

Tangu kuanzishwa kwake mkoani Kagera limekuwa likiwafunza watoto katika shule za msingi kila wilaya michezo midogo midogo ya kujenga ushirikiano wa pamoja hasa watoto wa kike kujiamini na kushirikiana zaidi na wenzao wa kiume.

Post a Comment

0 Comments