habari Mpya


KIGOMA-Simamieni Vyema Miradi ya REA ili kutimiza malengo ya Serikali.

26994092_2017314731879806_1589958551452772932_n
Waziri wa Nishati wa Tanzania, Dr Medard Kalemani mwenye miwani akizindua Mradi wa Umeme Vijijini (REA) awamu ya tatu Mkoani Kigoma, uzinduzi ambao umefanyika kwenye kijiji cha Mabamba Wilayani Kibondo mkoani Kigoma.Pembeni yake ni Viongozi mbalimbali wa Serikali na Chama na Wananchi wakishuhudia uzinduzi huo.
27067713_2017314698546476_2725236512744856073_n
Waziri wa Nishati wa Tanzania, Dr Medard Kalemani amewaagiza Viongozi wa Mkoa na  Wilaya za Kakonko na Kibondo sambamba na Meneja wa Shirika la Ugavi wa Umeme TANESCO kwenye wilaya hizo mkoani Kigoma kusimamia miradi ya umeme ya REA awamu ya tatu kwenye maeneo yao ili kutimiza malengo ya serikali. 
 
Dr Kalemani ametoa agizo hilo wakati wa uzinduzi wa mradi wa umeme vijijini (REA) awamu ya tatu Mkoani Kigoma, uzinduzi ambao umefanyika kwenye kijiji cha Mabamba Wilayani Kibondo.
27459833_2017314858546460_5586833735367797714_n
Amesema Serikali imetenga Shilingi Bilioni 60 kwa Miradi ya Umeme kwa Mkoa mzima wa Kigoma ambapo shilingi Bilioni 25 zimetengwa kwa wilaya za Kibondo na Kakonko hivyo viongozi hao wanapaswa kuwasimamia wakandarasi kuhakikisha wanafanya kazi kwa wakati.
 
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Generali Mstaafu Emmanuel Maganga amemuhakikishia waziri Kalemani kuwa ofisi yake itasimamia miradi hiyo kwa karibu huku akiwahimiza viongozi wa wilaya ya Kibondo kuwasimamia wakandarasi kwenye maeneo yao ili kutimiza malengo ya serikali ya kuwafikishia maendeleo wananchi.
27073076_2017314801879799_8773643683890176398_n

Post a Comment

0 Comments