habari Mpya


Taswira Picha Askofu Darlington Bendankeha Asimikwa Uaskofu Mkuu wa Kanisa Anglican Dayosisi ya Kagera.

Askofu Darlington Bendankeha Pichani akisaini Hati ya Kiapo chake cha Uaskofu kabla ya Kusimikwa kuwa Askofu Mkuu Kanisa la Anglican Dayosisi ya Kagera,mkoani Kagera.

Tukio la Kusimikwa limefanyika leo October 29, 2017 katika Kanisa la Anglican Murgwanza wilayani ngara mkoani Kagera , akiwa  ni Askofu wa nne wa Anglican Dayosisi ya Kagera iliyoanzishwa mwaka 1985 kutoka Dayosisi ya Viktoria Nyanza –Mwanza.
 
Ibada hiyo imehudhuriwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi akiwa Mgeni rasmi,Viongozi mbalimbali wa Serikali,Chama na Waumini wa Madhehebu mbalimbali kutoka Nchi Nzima.
 
Picha Na -Shaaban Ndyamukama.
Askofu Darlington Bendankeha akiungama wakati wa ibada ya Kusimikwa kuwa Askofu Mkuu Kanisa la Anglican Dayosisi ya Kagera,mkoani Kagera.
Askofu Darlington Bendankeha akiombewa kwa kuwekewa Mikono na Maaskofu wengine wakati wa ibada ya Kusimikwa kuwa Askofu Mkuu Kanisa la Anglican Dayosisi ya Kagera,mkoani Kagera leo October 29,2017.
Pichani Juu na Chini Askofu Mkuu wa Kanisa la  Anglican Tanzania, Jacob Chimeledya akimvika Msalaba wa Kiaskofu , Askofu Darlington Bendankeha  wakati wa ibada ya Kusimikwa kwake kuwa Askofu Mkuu Kanisa la Anglican Dayosisi ya Kagera,mkoani Kagera leo October 29,2017.

Askofu Darlington Bendankeha kushoto Pichani, akiwa na Fimbo ya Kichungaji baada ya Kusimikwa kuwa Askofu Mkuu Kanisa la Anglican Dayosisi ya Kagera,mkoani Kagera leo October 29,2017.

Askofu Darlington Bendankeha wa pili kutoka kushoto akiwa na Mkewe katika picha ya pamoja baada  ya Kusimikwa kuwa Askofu Mkuu Kanisa la Anglican Dayosisi ya Kagera,mkoani Kagera leo October 29,2017.Askofu Darlington Bendankeha akipongezwa na Mke wake  wakati wa ibada ya Kusimikwa kuwa Askofu Mkuu Kanisa la Anglican Dayosisi ya Kagera,mkoani Kagera leo October 29,2017.

Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi akisaini Kitabu cha Wageni wakati wa Hafla hiyo .


Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi akitoa neno wakati wa Hafla hiyo .Askofu Mkuu wa Kanisa la  Anglican Tanzania, Jacob Chimeledya pichani kulia akiwa na Askofu aliyestaafu ,Askofu Aaron Kijanjali kushoto kwake  wakati wa ibada ya Kumsimika  Askofu Mkuu mpya wa Kanisa la Anglican Dayosisi ya Kagera,mkoani Kagera leo October 29,2017 kwenye Kanisa Kuu la Murgwanza,wilayani Ngara mkoani Kagera.Picha juu na chini, ni  Maandamano ya Wachungaji,Waumini na Viongozi mbalimbali wakitoka  Kanisani kuelekea viwanja vya kanisa kuu la Murgwanza kwa ajili ya Ibada ya Kumsimika Askofu Darlington Bendankeha  kuwa Askofu Mkuu Kanisa la Anglican Dayosisi ya Kagera,mkoani Kagera leo October 29,2017.Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi akisalimia na Askofu aliyestaafu ,Askofu Aaron Kijanjali kushoto kwake.

Post a Comment

0 Comments