habari Mpya


Radi Yaua Ng'ombe Zaidi ya 30 wilayani Ngara,mkoani Kagera Leo October 13.

Wananchi wa kijiji cha Muhweza kata ya Mabawe wilaya ya Ngara mkoani Kagera wakichinja na kugawana nyama baada ya radi iliyoambatana na mvua kuwapiga ngombe 30 na kondoo saba Leo October 13,2017  majira ya saa 11 ambapo wenye ng’ombe hao wameamua wananchi wajichukulie nyama bure bila kuwauzia .
Picha/Habari na Shaaban Ndyamukama.

Zaidi ya Ng'ombe 30 na kondoo saba  wamekufa baada ya kupigwa na radi  jana    katika jijiji cha Muhweza kata ya Mabawe wilaya ya Ngara mkoani Kagera  ambapo radi hiyo  iliambatana na mvua majira ya saa 11 jioni kwenye kijiji hicho. 
 
Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Muhweza Bw.Alex Bahati Joseph amethibitisha kutokea kwa tukio hilo  na kwamba Ng’ombe hao walikuwa wanamilikiwa na wakazi wa kijiji cha Muhweza na Mukalehe  na  walikuwa pamoja malishoni.
 
Bw Joseph amesema wamiliki wa mifugo hiyo  waliopata janga hilo wameachia wanachi kujichukulia nyama bure  bila kuwauzia na hakuna daktari wa mifugo aliyefika jioni hiyo kutoa ushauri wa kitaalamu  juu ya uhalali wa kula nyama hiyo.

Matukio ya radi kuua  ng'ombe  na mifugo mingine wakiwemo wachungaji wa mifugo hiyo malishoni  na hata  binadamu wengineo hutokea kila mwaka katika wilaya za Ngara , Biharamulo, Muleba na Karagwe mkoani Kagera pia hata katika   wilaya inazounda mkoa  wa  Kigoma.

Post a Comment

0 Comments