habari Mpya


Mafuriko Dar yaua Watatu – RPC Mambosasa.

Mvua  zinazonyesha Jiji la Dar es Salaam Kama ilivyo kawaida, mvua hiyo iliharibu miundombinu ya usafiri ya maeneo kadhaa, ikisababisha baadhi ya barabara kutopitika na mitaro na barabara kadhaa kujaa maji.


 Picha zote na Iman NsamilaKAMANDA wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema watu watatu wamekufa kufuatia mvua kubwa zilizonyesha siku ya Alhamisi maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar.

Mambosasa ameyasema hayo jana October 27,2017, Ijumaa wakati akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Polisi Kanda Maalum.

 “Ikumbukwe kwamba usiku wa kuamkia jana, mvua kubwa ilinyesha na kusababisha mafuriko ambayo yameleta maafa ndani ya jiji letu, marufiko ambayo hayajatokea siku za hivi karibuni.

“Maeneo ya Tabata uliokotwa mwili mmoja wa kijana ambaye alisombwa na maji hayo, eneo la Mbezi Luis, gari lilitumbukia mtaroni ambako pia kifo kimoja kimeripotiwa kutokea, na mtoto mdogo amethibitika kufariki kutokana na mvua hizo.” alisema Mambosasa.

Aidha Mambosasa amesema madhara ya mali zilizoharibika bado jeshi hilo halijapata thamani yake huku akieleza kuwa hakuna majeruhi aliyeripotiwa kutokana na tukio hilo.

Post a Comment

0 Comments