habari Mpya


U-17 AFCON GABON 2017: Kundi B la Serengeti Boys latoka Sare.

Msimamo wa Kundi B- Timu ya taifa ya vijana wa Tanzania chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ imetoka suluhu (0-0) dhidi ya Mabingwa watetezi Mali katika mchezo wake wa kwanza wa Mashindano ya kugombea Ubingwa wa Afrika kwa Vijana chini ya Miaka 17, TOTAL U-17 AFCON GABON 2017, iliyoanza May 14,2017 kwa Mechi za Kundi A huko Nchini Gabon.

 Mechi hiyo ya Kundi B ilichezwa Stade de L’Amitle, Mjini Libreville huko Gabon.

Hapo Jana, Wenyeji Gabon walianza vibaya kwa kutandikwa magoli 5-1 na Guinea na kisha Ghana kuibonda Cameroun goli 4-1 zote zikiwa Mechi za Kundi A.

 Mchezo wa pili wa Kundi B kati ya Angola dhidi ya  Niger ulimalizika nao kwa matokeo ya sare ya bao 2-2.
Mashindano haya yataendelea tena Jumatano kwa Mechi za Kundi A na Serengeti Boys kushuka tena dimbani Alhamisi kuivaa Angola ndani ya Stade de L’Amitle, Mjini Libreville huko Gabon.

Washindi Wawili wa kila Kundi watatinga Nusu Fainali na Timu hizo 4 zitakazocheza Nusu Fainali ndizo hizo hizo zitafuzu kucheza Fainali za FIFA za Kombe la Dunia kwa Vijana U-17 huko Nchini India Mwezi Oktoba,2017.

TOTAL U-17 AFCON GABON 2017.

**Saa za Bongo

Jumatano May 17, 2017

KUNDI A

1730 Guinea v Cameroun [Stade de POG, Port Gentil]

2030 Ghana v Gabon [Stade de POG, Port Gentil]

Alhamisi May 18, 2017.

KUNDI B

1730 Tanzania v Angola [Stade de L’Amitle, Libreville]

2030 Niger v Mali [Stade de L’Amitle, Libreville]

Post a Comment

0 Comments