habari Mpya


Tujifunze Ujasirimali wa Diwani Baada ya Kustaafu-Geita.

Diwani mstaafu wa kata ya Muganza wilaya ya Chato mkoa wa Geita Michael Maduka (mwenye shati jekundu)  akiwa shambani na kibarua wake juzi  wakimwagilia bustani ya matikiti maji aliyoanzisha baada ya kupumzika siasa kwa kipindi kifupi kupitia Chadema  akitegemea kugombea udiwani kwa kata hiyo mwaka 2020.


Diwani huyo aliacha kugombea baada ya kusoma upepo kuwa katika kipindi kilichopita alishindwa kutekeleza ahadi yake ya kuwapatia wananchi wa kata hiyo huduma ya maji na zahanati ambapo alihamasisha ujenzi wa kituo cha Afya cha kata na kuishia renta kwa thamani ya sh 87 milioni

Akiongea na mwandishi wetu alisema amejikita katika kilimo cha bustani ya matunda na mbogamboga na ufugaji wa samaki pamoja na kuku kuongeza kipato kwake na familia lakini akilenga kukusanya fedha zitakazotumika kwenye kampeni mwaka 2020 atakapokuwa amejipanga kubainisha changamoto za wananchi baada ya kutathimini uwakilishi wa diwani aliyepo wa CCM Emanuel Tagota

Alisema kilimo cha bustani na ufugaji unamsaidia kupata fedha za kununua dawa za kuulia wadudu wanaoshambulia mazao mbalimbali lakini hata kununua chakula cha mifugo na dawa za magonjwa ya kuku ambapo kila wiki hukusanya tey 40 za mayai huku akiuza matikiti maji na nyanya kwa kuingiza Sh 2.3 kwa mwezi.

Picha na Shaaban Ndyamukama


Post a Comment

0 Comments