habari Mpya


Taarifa ya Habari ya Saa 24 zilizopita May 05,2017-Radio Kwizera FM-Ngara.

SOURCE: RK, EZ (kikao)
ED: FM
DATE: Friday, May 5, 2017

CHATO

Jamii Wilayani Chato Mkoani Geita imetakiwa kushirikiana na walimu wa shule za msingi na sekondari ili kudhibiti baadhi ya wanafunzi ambao hawafiki shuleni na badala yake kuishia njiani hali ambayo inachangia kushuka kiwango cha taaluma.

Hayo yamebainishwa na viongozi wa kata ya Buseresere  Wilayani humo  katika kikao cha maendeleo ya kata kilicho fanyika hivi karibuni ambapo  wamesema kuwa jamii inapaswa kutoa  ushirikiano kwa walimu wa shule  zote ili kukomesha tatizo hilo.

Akizungumza kwa niaba ya mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Buseresere baada ya kikao hicho kumalizika Bw Peter Yombo ambae ni mwalimu wa nidhamu katika shule hiyo amesema kuwa endapo wazazi na walezi watashirikiana kwa pamoja na walimu jambo hilo litakoma mara moja.

Insert………….mwalimu
cue in……………..
cue out……………

Aidha diwani wa kata ya Buseresere Bw Godfrey Mitti amewataka viongozi katika  kata hiyo kupitisha sheria ndogo ambayo itambana mzazi pamoja na mwanafunzi atakae kiuka sheria na taratibu za shule


SOURCE: RK, AE (Mkuu wa mkoa atoa agizo)
ED: FM
DATE: Friday, May 5, 2017

KIGOMA.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma brigedia jenerali mstaafu Emmanuel Maganga amemwagiza msimamizi wa bodi ya Kahawa kanda ya Kigoma Bw Melkiad  Massawe  kuhakikisha anatekeleza majukumu yake kikamilifu kwa kutoa elimu ya usimamizi na ukaguzi bora wa zao la hilo

Brigedia jenerali mstaafu Maganga ametoa maagizo hayo katika kikao cha wadau wa zao la Kahawa kilichofanyika mkoani humo na kujumuisha wakurugenzi wa halimashauri zote,wakuu wa wilaya,wenyeviti wa halimashauri, maafisa kilimo pamoja na baadhi ya wakulima wa zao hilo 

Bw Melkiad  Massawe ambae ni meneja na msimamizi wa bodi ya Kahawa kwa mikoa ya Mara, Kagera, Geita na Kigoma ametakiwa kuhakikisha anaitembelea mikoa yote aliyopangiwa na kutoa elimu kwa wakulima sambamba na maafisa wengine kwani zao la kahawa ni miongoni mwa mazao yanayoweza kuinua kipato cha mkulima 

Insert…………….Maganga
Que in……………..
Que out……………….

Wakizungumzia changamoto zinazowakabili katika uandaaji na uuzaji wa zao la kahawa baadhi ya wakulima akiwemo Bw Norasko John na Yahya Mahwisa wamesema ushuru unaotozwa na halimashauri, Bei kubwa ya miche na ukosefu wa elimu juu ya kilimo bora cha zao hilo vinapelekea wakulima wengi kushindwa kumudu kilimo cha zao hilo 


SOURCE: RK, LG (Hukumu)
ED: AG
DATE: Friday, May 05, 2017, 2017

NGARA

Mahakama ya wilayani Ngara mkoani Kagera imemuhuku Bw Jonasi Kaburu mwenye umri wa miaka 18 mkazi wa mtaa wa Nakatunga kutumikia kifungo cha mwaka mmoja gerezani au kulipa faini ya shilingi laki tatu kwa kosa la kujeruhi


Mwendesha mashitaka wa Jeshi la polisi wilaya Ngara Bw Respicus John ameiambia mahakama kuwa mnamo Mei 4 mwaka huu majira ya saa mbili usiku mshitakiwa alimjeruhi kichwani Bw Novatus Medani mwenye umri wa miaka 26 mkazi wa mtaa wa Nakatunga kwa kutumia kitu chenye ncha kali


Baada ya kusomewa shitaka lake mshtakiwa amekiri kutenda kosa hilo ndipo mahakama ikatoa adhabu hiyo ili kuwa fundisho kwa wengine


Mshitakiwa Jonasi Kaburu ameamua kutumikia kifungo cha mwaka mmoja gerezani baada ya kushindwa kulipa faini ya shilingi laki tatu


SOURCE: RK, wm (mradi wa chakula)
ED: AG
DATE: Friday, May 05, 2017, 2017

BUKOBA

Jumla ya kaya elfu tano katika wilaya tano za mkoa wa Kagera zilizoathirika    na tetemeko la ardhi pamoja na ukame mwaka jana, zinatarajia kunufaika na mradi wa shirika la chakula na kilimo la umoja wa mataifa  FAO  ambao utaghalimu zaidi ya shilingi milioni 600 

Mradi huo umezinduliwa leo na mkuu wa mkoa wa Kagera meja jenerali mstaafu Salum Kijuu katika ukumbi wa mkuu mkoa ambapo wakuu wa wilaya, wakurugenzi na wataalam wa kilimo na chakula kutoka wilaya za Bukoba, Muleba, Kerwa pamoja na Misenyi wameshiriki katika uzinduzi huo 

Meja  mstaafu Kijuu  amesema kuwa ofisi yake mwezi Januari mwaka huu imeandika barua katika shirika la kilimo na chakula la umoja wa mataifa kuomba mbegu kwa ajili ya kuwapatia wananchi  ambao  hadi sasa  wanakabiliwa na ukosefu wa mbegu kwa ajili ya kuzalisha mazao  mbalimbali ikiwemo viazi na kunde  

Insert… MSTAAFA KIJUU
Cuein ….Shirika la kilimo na chakula
Cueout …..usimpe mtu samaki mpe nyavu

Kwa upande wake   mwakilishi  wa shirika la  chakula  na kilimo la umoja wa mataifa hapa nchini Bw Charles Tolai amesema kuwa wilaya zitakazonufaika na mradi huo ni Kyerwa, Misenyi, Muleba, Manispaa ya Bukoba na halmashauri ya Bukoba na  utadumu kwa kipindi cha miaka miwili hadi mwaka 2020


SOURCE: RK, KK (ges)
ED: FM
DATE: Friday, May 5, 2017

MWANZA
Meneja wa wakala wa vipimo Mkoa wa Mwanza Hemedy Kipengele amewataka wananchi Mkoani humo kuhakikisha wanapima kiasi cha ujazo wa gesi iliyopo kabla ya kununua kwa wakala yeyote ili kuepuka kuibiwa

Amebanisha hayo wakati akiongea na radio kwizera kwa njia ya simu kufuatia malalamiko ya baadhi ya wananchi wa jiji la mwanza juu ya kuuziwa gesi na kuisha kwa muda mfupi licha ya kutokuwa na matumizi makubwa

Amesema tayari wameanza kuchukua hatua kwa kukagua mawakala wote ndani ya jiji la Mwanza wanaouza gesi za majumbani ili kuhakikisha kila mmoja anakuwa na mzani huku akibanisha kuwa atakayebainika hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake

Awali baadhi ya wananchi wa jiji la Mwanza wamelalamikia juu ya kampuni zinazotoa huduma ya uuzaji wa gesi ya matumizi ya majumbani kuibiwa gesi kutokana na kutojua ujazo halisi hali inayaosababishwa na uuzaji bila kutumia mzani


SOURCE: RK, DT (bunge)
ED: AG
DATE: Friday, May 05, 2017, 2017

DODOMA

Wizara ya elimu, sayansi na teknolojia imeweka mkakati wa kuimarisha elimu ya watu wazima kwa kuandaa mwongozo wa wawezeshaji na utekelezaji ili watu wazima wasiojua kusoma na kuandika wajiunge 

Naibu waziri wa elimu, sayansi na teknolojia Bi Stella Manyanya amebainisha kuwa kila mamalaka ya serikali ya mitaa imeelekezwa kutenga fedha katika bajeti zake kwa ajili ya kununua vifaa vya kujifunzia na kufundishia na kutoa mafunzo kwa wawezeshaji

Bi  Manyanya  amesema kuwa kwa kutambua umuhimu wa watu wazima kujua kusoma na kuandika, serikali imeanzisha mpango wa uwiano kati ya elimu ya wa watu wazima na jamii MUKEJA  ambao umeshaanza kutumiwa kama majaribio katika wilaya tisa 

Isert…….waziri Manyanya
cue in…….serikali imekuwa ikitenga fedha
cue out……Temeke na Ilala

Bi Manyanya ameongeza kuwa wizara hiyo imetoa kipaumbele na kuweka mikakati katika suala zima la kutokomeza ongezeko la watu wasiojua kusoma na kuandika ili kujenga taifa la wasomi ifikapo mwaka 2025  


SOURCE: RK, LT (Afya)
ED: FM
DATE: Friday, May 5, 2017

KINSHASA

Madaktari kwenye hospitali za serikali kote nchini DRC wameingia katika mgomo wa siku tatu bila kuhudumia wagonjwa ili kushinikiza serikali ya DRC kutoa ulinzi wa kutosha kwa madaktari baada ya kifo cha daktari mmoja katika mji wa Uvira mashariki mwa DRC 

Kwa mujibu wa tangazo ambalo limetolewa jana na kamati tendaji ya madaktari nchini DRC limetaja kuwa mgomo huo unalenga kushinikiza serikali kutoa ulinzi kwa madaktari na wahusika wa mauaji ya Dr Gildo Byamungu ambaye ameuawa kwa kupigwa risasi mjini Uvira wafikishwe mahakamani

Katibu mkuu wa kamati tendaji ya madaktari nchini DRC Dr Monkoy Badjoky amesema katika muda wa siku tatu hakuna daktari atakaetoa huduma kwenye hospitali za serikali huku ameomba serikali kufanya liwezekanalo ili waliohusika na kifo cha Dr Byamungu wafikishwe mahakamani na hukumu dhidi yao itolewe

Mwishoni mwa mwezi uliopita Dr Byamungu ameuawa na watu wasio julikana kwa kupigwa risasi nyumbani kwake mauaji ambayo yamezusha ghasia katika mji wa Uvira na Bukavu ikiwa mpaka sasa mtu mmoja anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo

Post a Comment

0 Comments