habari Mpya


Soma Taarifa ya Habari ya Saa 24 zilizopita May 08,2017-Radio Kwizera FM-Ngara.

Picha na Maktaba Yetu.

SOURCE: RK, WM (vyeti feki)
ED: FM
DATE: Monday, May 08, 2017

KERWA.

Mkuu wa Wilaya ya Kerwa Mkoani Kagera Kanali mstafu Shabani Lisu amesema Wilaya yake  ina upungufu  wa watumishi wa idara ya afya  baada ya serikali kutangaza  kuwaondoa  watumishi wenye vyeti  feki  Wilayani humo 

Kanali mstaafu  Lisu  amesema hayo wakati akiongea na radio kwizera  juu ya upungufu  uliojitokeza  katika Wilaya  yake  kutokana na zoezi la kuwaondoa  watumishi  wenye vyeti feki ambapo watumishi waliopatikana na vyeti  feki ni 28 kati ya hao  16 wanatoka idara ya afya

Amesema  serikali  inapaswa kuangalia kwa jicho la huruma ili kupeleka  watumishi  wengine  hasa kitengo cha idara ya afya  kutokana  na upungufu  uliojitokeza baada ya kuwaondoa watumishi wenye vyeti feki  16  ili wagonjwa na jamii ya Kerwa waweze kupata huduma za afya 

Insert………….. Kanali Lisu
Cue in ……
Cue out …….

Hata hivyo Kanali Lisu amesema tayari wameshachukua hatua kwa kutoa taarifa kwa mamlaka husika ili serikali ikiajiri watumishi waweze kupangiwa Kerwa ambayo kwa sasa inaupungufu mkubwa wa watumishi wa kitengo cha idara ya afya

SOURCE: RK, SN (Elimu)
ED: FM
DATE: Monday, May 08, 2017

MULEBA

Wakazi wa kata ya Bisheke Wilayani Muleba Mkoani Kagera wameanza mkakati wa kujenga vyumba viwili vya madarasa ya shule ya msingi Katanda ambapo halmashauri ya Wilaya hiyo imechangia fedha kiasi cha shilingi milioni nane

Diwani wa kata ya Bisheke Bw Alexander Tinamanyile amesema hayo katika kikao cha baraza la madiwani wakati akiwasilisha taarifa ya kata hiyo kuhusu utekelezaji wa miradi ya maendeleo na changamoto zinazowakabili wananchi

Bw Tinamanyile amesema wakazi wa kata hiyo pia wanaendelea na ujenzi wa   vyumba   vya madarasa ya shule ya msingi Mulambi, Kabuga, Ichwandimi pamoja na nyumba ya mwalimu shule ya msingi Kiyebe ikiwemo umaliziaji wa vyumba vya madarasa ya shule ya msingi Mujunwa vilivyoezuliwa na upepo

Insert ………..Diwani Bisheke
Cue In ----Tunamalizia vyumba vilivyoezuliwa na upepo
Cue out ------tatizo ni umbali wa maeneo

Aidha diwani huyo ameiomba halmashauri kutengeneza barabara za vijiji na kata mbalimbali Wilayani humo ili kuharakisha usombaji wa vifaa vya ujenzi wa miradi ya wananchi na kuweza kupatikana huduma bora za kijamii wilayani humo

SOURCE: RK, em (Ameoteshwa aolewe na mchungaji)
ED: AG
DATE: Monday, May 08, 2017

KARAGWE

Mwanamke mmoja wilayani Karagwe mkoani Kagera ameitelekeza familia yake na kuolewa na Mchungaji kwa madai kuwa ameoteshwa kuolewa nae

Mwanamke huyo Bi Domina Damiani ameolewa na Mchungaji wa Kanisa la Huruma katika Kristo   Japhet Josepha lilipo katika kijiji cha Nyabwengira kata ya Ndama wilayani Karagwe

Akizungumza kanisa hapo mbele ya Kikosi cha ulinzi na usalama ambacho kimeongozwa na mkuu wa wilaya ya Karagew Bw godfrey Mheluka pamoja na kamati ya amani na maadili Bi Damiani amesema ameamua kuolewa kwa kuwa ni agizo la Mungu

Amesema kabla ya kuolewa na mchungaji huyo alikuwa ni muumini wa kawaida katika kanisa hilo na amefanikiwa na mume wake Donath Applo kuzaa watoto wanne lakini kila akilala amekuwa akioteshwa akihudumia nyumba ya mchungaji kama mama mchungaji

Insert………………….. Bi Damiani
Cue in………………..Ikatokea mara nyingine
Cue Out……………..Nikatoka kwenye usingizi

Awali Mkuu wa wilaya ya Karagwe Bw Godfrey Mheluka amesema kuwa ameamua kufika kanisani hapo mara baada ya baba wa mwanaume aliyemuoa mwanamke huyo mzee Apllo Fundi kufika ofisini kwake kumshitaki mchungaji kuwa amemuoa mama huyo bila kurudisha mahali

SOURCE: RK, Elias Z(mahojiano)
ED: AG
DATE: Monday, May 08, 2017

CHATO

Baadhi ya wananchi wa kata za Buseresere na Muungano zilizopo wilayani Chato mkoani Geita wamevitaka vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini kuhakikishavinatoa habari zake kwa  usahihi na kwa wakati pasipo kuipotosha jamiii

Wakiongea na radio kwizera kwa nyakati tofauti baadhi ya wananchi hao Bw Braiton Elia, Kipoloda John na Bw Gervas Tino wamesema kuwa  taarifa inapotolewa na kutangazwa inampa fursa mwananchi pamoja na serikali kujitathimini juu ya kile kinachokuwa kimetangazwa

Kwa upande wao wasikilizaji wa Redio kwizera kutoka kata ya Muungano wameipongeza radio kwizera kwa kuibua kero zinazowakabili na kuzitangaza kwa wakati bila kupotosha ukweli hali waliyobainisha kuwa ni chanzo cha maendeleo ndani ya wilaya ya Chato

Insert………………………WANANCHI
Cuein…………………..
Cueout………………….

Katika hatua nyingine wananchi hao wamewataka wamiliki wa vyombo vya habari kuhakikisha wanaboresha maslahi ya watumishi wao yatakayowapatia moyo wa kuendelea kutoa habari zenye matokeo chanya katika jamiii

SOURCE: RK, ak [mazingira]
ED: AG
DATE: Monday, May 08, 2017

MISSENYI

Halmashauri ya wilaya ya Missenyi mkoani Kagera imedai kuwa itawawajibisha wasimamizi wa ujenzi wa zahanati na shule zilizoangushwa na tetemeko la ardhi ambao watashindwa kuonesha thamani halisi ya fedha iliyotumika kwenye ujenzi au ukarabati wa miundombinu hiyo

Onyo hilo limetolewa na mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya hiyo Bw Limbe Moris akizungumza na watendaji na kwamba kimeundwa kikosi kazi ambacho kimepewa jukumu la kuhakikisha kinafuatilia matumizi ya fedha na vifaa vilivyotolewa kwenye taasisi husika kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu

Amesema kuwa endapo wasimamizi wa taasisi watashindwa kutoa thamani halisi ya fedha watawajibika na kwamba kwa taasisi zitakazokuwa na vifaa ambavyo havijatumika ikiwemo simenti watavichukua na kuvihamishia kwenye ujenzi wa shule za sekondari Minziro na Mwabuki za kidato cha 5 na 6.

Insert..........limbe moris
Cue in........kama ni shule
Cue out........iabidi ujibu

Kwa upande wao baadhi ya wakazi wa wilaya ya Missenyi Allen Abdon na Zakalia Sande wamepongeza uamuzi huo wa halmashauri wakidai zipo baadhi ya taasisi ambazo zimeharibiwa na tetemeko na kupewa msaada wa vifaa lakini hazijakarabatiwa wakidai fedha za mafundi hawanaWasiliana/News Desk, Ngara Kagera.
Chief News Editor
Ms AuleriaGabriel
auleria@radiokwizera.com
Mobile: +255 769722554

Post a Comment

0 Comments