habari Mpya


Simon Kanguye – ''..Kuhamisha Mwalimu lazima Ulipwe Kwanza.’’


Wanafunzi wa Shule ya Msingi Nabuhima,Wilayani Kibondo,Kigoma.

Baadhi ya Walimu wa Shule za Msingi  Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma, waliohamishwa vituo vipya vya kazi wameshindwa kufika katika vituo  walikohamishiwa baada ya Halmashauri ya Wilaya kushindwa kuwalipa stahiki zao.

Wakiongea na Wanahabari  jana,May 10,2017 baadhi ya Walimu hao amabo ni Anna Bakari aliyekuwa Anafundisha Shule ya Msingi  Kibondo nakuhamishiwa Kigendeka  na Anthon Sakala alikuwa vile Kibondo na kuhamishiwa shule ya Msingi Kahama walisema kuwa  walipewa barua za uhamisho tangu febuary 17,mwaka huu, lakini hadi May 11,2017 hawajalipwa pesa za usumbufu na za kusafirisha mizigo yao kama taratibu zinavyoelekeza badala yake wanaambiwa wajisafirishe wenyewe.
Kaimu Mkurugenzi wilaya ya Kibondo-Mhe Gabriel Chitupila.

‘’Kila tunapoenda kumuona mwajili wetu ili tupewe stahiki zetu, tunaambiwa tujisafirishe malipo yote baadae na hapa tuko mitaani na jambo ili si jema maana kanuni zinasema mfanyakazi anapohamishwa lazima alipwe pesa za usumbufu, na safari toka kwa mwajili’’ alisema Anthon

Sakata hilo lilihamia katika Baraza la Madiwani kwenye kikao cha robo ya tatu kilichofanyika jana  ambapo Mhe. Razalo Piter, Diwani kata ya Busunzu alitaka kufahamu hatima ya walimu hao na wanafunzi mashuleni ambao awapati huduma za masomo mashule kwa muda mrefu huku kaimu mkurugenzi wa halmashauri hiyo Gabriel Chitupila akidai atawachukulia hatua walimu wote ambao hawajaripoti vituon kwao kwani walisha taarifiwa kuwa watalipwa.
Mhe.Simon Kanguye .

Mhe.Simon Kanguye ,Mwenyekiti wa halmashauri hiyo alimtaka Mkurugenzi  kulitazama upya swala la kuwahamisha Walimu hao kwani linafanyika bila kuwepo bajeti ya kufanya hivyo na nilazima Walimu walipwe ili waende kwenye vituo vyao vya kazi.
Mbunge wa Jimbo la Mhambwe,Mhe. Atashasta Nditiyae.
Bw.Ntilo Nzigu,Mwenyekiti CWT- Kibondo.

Mwenyekiti wa Chama cha Walimu wilayani Kibondo Bw.Ntilio Nzigo alisema kuwa hali hiyo inawahathili walimu kisaikolojia kwa kulingana na zoezi la kuhakiki vyeti udhaniwa nao wamo ndani ya kundi la wafanyakazi waliogushi au watumishi hewa na kulingana na idadi kubwa ya walimu 129 kuwa mitaani ni kuathili hali ya taaluma mashuleni kwani wanafunzi hawafundishwi kwa siku hi ambazo walimu wako mitaani.
Bi.Anna Bakari- Mwalimu.

Bw.Anthon Sakala -Mwalimu.
Bw.Lyaki Majo- Katibu CWT- Kibondo.

Alipotakiwa kueleza hali halisi, Katibu wa chama cha Walimu Kibondo, Bw. Lyaki Majo alisema walimu wengi na wanashinda mitaani na kila wanapo jaribu kudai upewa vitisho vya kufukuzwa kazi jambo ambalo ni kuwanyima haki  huku mbunge wa Jimbo la Mhambwe, Mhe. Atashasta Nditiyae akimtaka mkurugenzi kuwarudisha walimu watatu waliiosimamishwa kazi

Haiwezekani serikali inahangaika kutaka kuajili walimu huku wengine wanafukuzwa bila utaratibu hili si jema bali zifuatwe taratibu za kazi’’ alisema Nditiye.

Habari/Picha na -Muhingo Mwemezi.

Post a Comment

0 Comments