habari Mpya


EPL 2016/2017-Chelsea Kuutangaza Ubingwa Ijumaa wakiishinda West Bromwich Albion.

Timu ya Chelsea imeendelea kujikita kileleni mwa Ligi Kuu England 2016/2017 baada ya kuitwanga Middlesbrough Bao 3-0 na kuishusha Daraja huku wao wakisubili ushindi kwenye Mechi moja tu ili watwae Ubingwa huo wa Ligi.

 Sasa Chelsea wanaweza kuwa Mabingwa Ijumaa May 12,2017 wakiwa na mechi 2 mkononi ikiwa watashinda Ugenini huko The Hawthorns watakapocheza na West Bromwich Albion.
Chelsea walifunga Bao lao la Kwanza Dakika ya 23 kwa Pasi safi ya Cesc Fabregas na Diego Costa kukwamisha Mpira Wavuni.

Bao la Pili la Chelsea liliingia Dakika ya 34 Mfungaji akiwa Marcos Alonso aliemalizia Krosi ya Azpilicueta.

Dakika ya 65 alikuwa tena Cesc Fabregas aliemsukia Nemanja Matic kupiga Bao la 3 na Chelsea kuongoza 3-0 Bao zilizodumu hadio mwisho.
Matokeo haya ya nyumbani Stamford Bridge, Jijini London, yamewaunganisha Middlesbrough,Pichani maarufu kama Boro pamoja na Sunderland kuteremshwa Daraja na sasa watacheza Daraja la chini ya EPL, la Championship, Msimu ujao.

LIGI KUU ENGLAND-2016/2017.

Ratiba

Jumatano Mei 10,2017.

2145 Southampton v Arsenal              

Post a Comment

0 Comments