habari Mpya


WATAWA WOTE ULIMWENGUNI WAUNGANA KUSHEREKEA SIKU YA KUTOLEWA BWANA HEKALUNI: Siku ya Watawa duniani

WATAWA WOTE ULIMWENGUNI WAUNGANA KUSHEREKEA SIKU YA KUTOLEWA BWANA HEKALUNI: Siku ya Watawa duniani

PICHA NA BOB MOLIS

Siku kuu ya Kutolewa Bwana Hekaluni: Siku ya Watawa Duniani

Pichani ni baadhi ya Wata wa kanisa katoli wilayani Ngara katika maadhimisho ya siku ya kutolewa Bwana Hekaluni sambamba na siku ya Watawa ambayo inasherekewa na Watawa wote ulimwenguni kote.

Maadhimisho ya Siku ya Watawa Duniani ni fursa ya kuangalia matumaini ya ongezeko la miito ya kitawa ndani ya Kanisa; changamoto mbali mbali zinazoendelea kujitokeza katika ulimwengu wa utandawazi na maendeleo ya sayansi na teknolojia pamoja na umuhimu wa ushuhuda wenye mvuto na mashiko kutoka kwa walezi waliokabidhiwa dhamana na jukumu la kuwasindikiza vijana!

Kila tar 2 februali katika kanisa katoliki ni siku ya 40  baada siku ya noeli na ni siku ya kutolewa bwana hekaluni sambamba na kuadhimisha siku ya  wanamaisha ya wakfu duniani kote .maadhimisho hayo yalifanyika  katika kanisa la Mt. fransisko wa asizzi mjini ngara  ,nakuwakutanisaha  mashirika mbalimbali ya Watawa wakike na wa kiume wanaofanya utume wao katika  dekania  ya ngara jimbo katoliki la rulenge ngara
Maadhimisho hayo yaliongozwa na vika wa watawa padre inyas kwizigizya yalifunguliwa kwa kubariki mishumaa ambayo ni alama ya kristo mwenyewe aliye mwanga  wa mataifa nasi kwa namna ya pekee wazazi wetuw ametutoa hekaluni kufanya kazi ya bwana


Post a Comment

0 Comments