habari Mpya


Simba yaendelea kujikita Kileleni, Yanga yavutwa shati Taifa.

Klabu ya Simba imeibuka na ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya timu ya Mtibwa Sugar  ya mjini Morogoro na kuifanya kufikisha alama 53 na hivyo kuendelea kujikita kileleni mwa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Katika mchezo huo wa Ligi Kuu soka Tanzania bara mzunguko wa mwisho, Simba ilipata mabao yake kupitia nahodha John Bocco,beki Mohamed Hussein na kiungo Hassan Dilunga.

Upande wa Mchezo wa Yanga dhidi ya Mbeya City mchezo uliochezwa uwanja wa Taifa, Yanga wamelazimishwa sare ya 1-1 na Sare hiyo inazidi kuwatoa Yanga SC kwenye mbio za ubingwa, kwani wakifikisha pointi 38 katika mchezo wa 19 wanazidiwa pointi sita na Azam FC na pointi 12 na mabingwa watetezi, Simba SC.

Katika mchezo wa leo, Mbeya City waliitangulia Yanga SC kwa bao la kujifunga la beki Mghana, Lamine Moro aliyekuwa anajaribu kuutoa nje mpira uliopigwa na Rehani Kibingu dakika ya 41.

Post a Comment

0 Comments