habari Mpya


Rais Mstaafu wa Kenya Daniel Arap Moi Afariki Dunia.

Daniel Arap Moi, rais wa pili wa Kenya ameaga dunia leo Jumanne,February 4,2020. Kifo chake kimetangazwa na Rais Uhuru Kenyatta, katika tangazo lililorushwa moja kwa moja na televisheni ya taifa.

"Kwa masikitiko makubwa natangaza kifo cha kiongozi mkubwa Afrika, Daniel Toroitich arap Moi, rais wa pili wa Kenya. Raisi mstaafu amefariki katika Hospitali ya Nairobi mapema asubuhi ya leo Februari 4 akiwa na familia yake.  -Amesema

Mzee Moi alizaliwa Septemba 2, 1924 na alitawala Kenya kwa miaka 24 kutoka 1978 mpaka 2002.

Tangazo hilo kutoka Ikulu limesema kuwa mzee Moi, hata baada ya kuondoka madarakani aliendelea kulitumikia taifa la Kenya na Afrika kwa kuwafundisha viongozi wa Kenya na nje ya Kenya, akiendelea kushiriki kwenye maendeleo ya miradi mbalimbali na kazi za misaada akiihubiri amani, upendo na umoja barani Afrika na duniani.

Post a Comment

0 Comments