habari Mpya


Mkurugenzi wa Rado Kwizera azungumzia faida za Radio Kwizera katika jamii

Habari na Auleria Gabriel
Picha na Bob Maurice
Asasi isiyokuwa ya kiserikali ya Young Lawyers Foundation yenye makao yake jijini Dar es salaam, imeanza kutoa mafunzo yatakayodumu kwa siku tatu kwa baadhi ya wadau wanaouzunguka Mradi wa ujenzi wa kufua umeme wa maji Rusumo uliopo katika kijiji cha Rusumo wilayani Ngara mkoani Kagera.

Mafunzo hayo yanayofanyika kuanzia Februari 17 hadi 19 mwaka huu, yanahusisha wananchi, viongozi wa serikali na dini kutoka vijiji vitatu vya Kyenda, Mshikamano na Rusumo pamoja na wafanyakazi kutoka kandarasi mbili zinazofanya ujenzi katika eneo hilo
Mafunzo haya yanafadhiliwa na kampuni ya  NELSAP ambayo ndiyo inaimamia ujenzi wa mradi huo wa umeme.

Lengo la mafunzo hayo ni kutaka jamii iwe na uelewa juu ya masuala ya ukatili wa kijinsia na pia iweze kutoa taarifa ikiwa kuna viashiria vyovyote vya ukatili wa kijinsia na udhalilishaji wa kingono vinavyojitokeza wakati mradi huo ukiendelea.

Akitoa mafunzo hayo, wakili wa mahakama kuu ya Tanzania na mkurugenzi wa asasi ya Young Lawyers Foundation, Bw. Jacob Mogendi amesema wamepewa jukumu la kutoa mafunzo hayo na kampuni ya NELSAP, lengo ikiwa ni kupambana na mitazamo hasi ndani ya jamii inayosababisha uweo wa unyanyasaji wa kijinsia na kingono.
Naye Bw. Gaspar Mashingia ambaye ni Afisa maendeleo ya jamii na Makazi katika mradi wa umeme wa Rusumo kutoka kampuni ya NELSAP anasema, mafunzo haya yatakuwa na mchango mkubwa kuhakikisha mradi huo unakamilika bila kuwepo na matukio ya ukatili wa kijinisia na kingono eidha kwa wafanyakazi ama jamii kwa ujumla.
Nao Baadhi ya wadau walioshiriki mafunzo haya wameeleza kuwa, elimu hii waliyoipata itasaidia kwa kiasi kikubwa kuzuia vitendo vya ukatili wa kijinsia na  kingono katika maeneo yao.

Mradi wa ujenzi wa kufua umeme wa maji Rusumo wenye megawati 80, unatekelezwa kwa ushirikiano wa nchi za Tanzania, Burundi na Rwanda ambapo kila nchi itapata megawati 27
Mradi huu ulioanza tangu mwaka 2017, unatarajiwa kugharimu dola milioni 468 za kimarekani na unafadhiriwa na wadau wa maendeleo ambao ni Benki ya Maendeleo Afrika (AfdB) na Benki ya Dunia 

Post a Comment

0 Comments