habari Mpya


Mapato ya ndani Halmashauri Ngara Yapanda kwa Zaidi ya Bilioni 4.

Afisa Elimu Sekondari wilaya ya Ngara,Bw. Ntakisigaye George akimkabidhi zawadi za ufaulu wa kidato cha nne za Shule ya Sekondari Lukole Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Mhe.Eric Nkilamachumu(kushoto) na katikati ni Kaimu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Ngara Mhe. Wilibadi John Bandala. 

Na Asma Ahmed –RK Ngara.

Mapato ya ndani ya Halmashauri ya wilaya ya Ngara mkoani Kagera yamepanda kutoka bilioni 39, milioni 317, laki 5, elfu 40 na 994 hadi kufikia bilioni 43, milioni 704, laki 9, elfu 70 na 443 sawa na ongezeko la zaidi ya bilioni 4.

Kaimu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Ngara Bw. Wilibard Bambala amesema hayo baada ya kumalizika kwa kikao cha baraza la madiwani cha kujadili mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha wa 2020/2021 kilichofanyika katika ukumbi wa halimashauri hiyo.

Aidha amesema ongezeko la mapato hayo ni kutokana na ushuru unaokusanywa katika vyanzo vya mapato wilayani humo pamoja na ruzuku kutoka Serikalini.

Pamoja na hayo, Mhe. Bambala pia amewataka madiwani wa halmashauri ya Ngara kuhakikisha bajeti ya fedha ambayo itakuwa ikitolewa katika kata zao isimamiwe vizuri ili kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

Post a Comment

0 Comments