habari Mpya


Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa CCM Imemfukuza Uanachama Waziri wa Zamani wa Mambo ya Nje, Bernard Membe.

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa CCM ikiongozwa na Mwenyekiti na Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli imeazimia kumfukuza uanachama Bw.Bernard Membe. 

Kikao hicho cha kawaida kimeketi Ijumaa,February 28,2020 Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba, Dar es Salaam.
Wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa wakiongozwa na Mwenyekiti  Rais John Magufuli wakiwa katika kikao cha kawaida cha Kamati Kuu kinachoendelea katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba, Dar es salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habri, Katibu wa Itikadi na uenezi wa CCM, Bw.Humphrey Polepole katika mkutano na waandishi wa habari alieleza uamuzi wa kamati kuu ambayo ilitoa siku saba kwa kamati ya nidhamu iliyowahoji vigogo hao kukamilisha suala lao na kuwasilisha taarifa.

Wakati Bw.Membe akivuliwa uanachama, Katibu mkuu wa zamani wa CCM, Bw.Abdulrahman Kinana amepewa karipio na kutakiwa kutogombea nafasi yoyote ndani ya chama hicho kwa miezi 18 huku Katibu Mkuu mwingine wa zamani, Bw.Yusuf Makamba akisamehewa.

Dakika chache baada ya Kamati Kuu ya CCM kumvua uanachama Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje, Bw.Bernard Membe, ameibuka kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter na kusema watanzania watulie atapata muda wa kuongea muda si mrefu.

Post a Comment

0 Comments