habari Mpya


Basi la Premier Line Lagongana na Lori.

Basi la kampuni ya Premier Line linalofanya safari zake kati ya Mwanza na Mbeya limegongana uso kwa na lori lenye namba za usajili T486 ANU ambalo lilikuwa likivuta tela lenye namba T 775 APT, maeneo ya Inyala, Mbeya Vijijini leo Ijumaa, Feb. 7, 2020, asubuhi.
Daktari wa Kitengo cha Dharura katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya, Dkt. Olivia Masoi amethibitisha kupokea majeruhi 10 wa ajali hiyo, ambapo amesema watu 2 waliodhaniwa kuwa wamekufa katika eneo la Ajali wako hai.

Post a Comment

0 Comments