habari Mpya


Yanga SC yaungana na Simba SC Hatua ya 16 Bora Kombe la TFF.

Kwa matokeo hayo juu , Yanga SC inaungana na vigogo wenzao, Simba SC kutinga hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC).

Kwa ushindi huo, Yanga SC watamenyana na Gwambina FC ya Daraja la Kwanza ambayo imeitoa Ruvu Shooting kwa penalti 7-6 baada ya sare ya 1-1 Uwanja wa Gwambina, Misungwi.

Lipuli FC imekuwa timu nyingine ya Ligi Kuu kutolewa baada ya Mtibwa Sugar na Ruvu Shooting kufuatia kufungwa kwa penalti 5-4 baada ya sare ya 2-2 na Kitayosa Uwanja wa Samora mjini Iringa.
Kitayosa FC, Namungo FC, Kagera Sugar, Stand United  na Yanga SC zinaungana na Alliance FC, Ndanda SC, Ihefu FC, JKT Tanzania, Simba SC, Gwambina FC na Sahare All Stars, KMC, Panama na Mbeya City kuingia raundi ya tano ya michuano hiyo ambayo bingwa wake hucheza michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Hatua ya 32 Bora itahitimishwa leo Jumatatu January 27,2020 kwa mabingwa watetezi, Azam FC kumenyana na Friends Rangers Dar es Salaam.

Post a Comment

0 Comments