habari Mpya


Yanga SC Kulitafuta Kombe la Mapinduzi 2020 January 9 mbele ya Mtibwa Sugar.

Yanga SC imefanikiwa kutinga Nusu Fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi 2020 baada ya kupata ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Jamhuri ya Pemba usiku wa January 7, kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Ushindi wa Yanga SC , umetokana na mabao ya nyota wake Kizanzibari, beki Adeyoum Saleh Ahmed dakika ya 45 na ushei na kiungo Mohammed Issa Juma ‘Banka’ dakika ya 85.

Sasa Yanga SC itamenyana na Mtibwa Sugar ya Morogoro Alhamisi January 9,Saa 2:15 usiku katika Nusu Fainali Uwanja wa Amaan.

Mtibwa yenyewe iliitoa Chipukizi ya Pemba kwa penalti 4-2 baada ya sare ya 1-1 kwenye Uwanja wa Gombani.

Post a Comment

0 Comments