habari Mpya


Vyombo vya habari nchini vijikite kuhabarisha umma kwa kutumia vifaa vya Teknolojia kufikisha taarifa kwa haraka kwenye jamii

HABARI NA AULERIA GABRIEL, ZANZIBAR
Inaelezwa kwamba ikiwa vyombo vya habari nchini vitajikita katika kuhabarisha umma kwa kutumia vifaa vya Teknolojia, Habari na Mawasiliano (TEHAMA) vinaweza kupiga hatua kubwa katika kuifikishia jamii taarifa kwa haraka
Hata hivyo kwa kutambua umuhimu wa TEHAMA katika sekta ya Habari nchini, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) chini ya Ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uswis (SDC) sasa linatoa mafunzo kwa waandishi wa habari kutoka redio 25 za kijamii Tanzania bara na Visiwani, mafunzo yanayodumu kwa siku 5 kuanzia Janurari 22 hadi 26 mwaka huu ambayo yanafanyikia katika ofisi za TAMWA Visiwani Zanzibar.

Akizungumza wakati akitoa Mafunzo hayo, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Tumaini jijini Dar Es Salaam Bw. Ajuaye Mdegela amesema kwa kutumia vifaa vya TEHAMA ni rahisi kuwafikiwa watu wengi hasa wa vijijini ambao wanakuwa vyanzo vya habari na wao wakatapa habari kwa haraka.
“Ukiangalia vyombo vya habari kwa sasa, havijafanya juhudi za kutosha kutumia TEHAMA kuwafikia jamii hasa kwa upande wa kutafuta habari, lakini ni rahisi kwenda kwa kasi na kwa eneo kubwa zaidi duniani kote. Kwahiyo, kutumia TEHAMA na vifaa vya TEHAMA tuna uwezo wa kuwafikia watu wengi kuliko kutumia mawimbi tuliyoyazoea.” Amesema Bw. Mdegela.
Redio za Jamii zinazoshiriki Mafunzo hayo kutoka Tanzania bara na Visiwani ni pamoja na Radio Kwizera FM, Orkonerei Fm Radio, Nuru Fm, Pambazuko Fm, Kahama FM, Loliondo Fm, Mpanda Radio, Uvinza Fm, Kitulo FM, Micheweni Fm, Chai Radio Rungwe, Sengerema Radio, Boma Hai Fm, Radio Fadhila, Mtegani Fm, Mazingira Radio, Ileje Fm, Ruangwa Fm, Storm Fm, Tumbatu Fm, Triple A Radio, Dodoma FM, Jamii Fm na Radio Pangani.

Post a Comment

0 Comments