habari Mpya


Ujenzi Hospitali ya Wilaya ya Chato Washika Kaisi.

Ujenzi wa majengo matano katika Hospitali ya Wilaya ya Chato Mkoani Geita umeanza, majengo yanayojengwa ni pamoja na wagonjwa wa nje ( OPD), jengo la Maabara, jengo baba, mama na mtoto (RCH), jengo la wazazi na sehemu ya kuchomea taka.

 Ujenzi huo unatarajiwa kugharimu shilingi bilioni 1.
Hapa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chato,Bw. Eliurd Mwaiteleke ameungana na mafundi kuhakikisha kazi inaenda kwa kasi. 
Aidha kukamilika kwa upanuzi huo wa majengo ya hospitali ya wilaya ya Chato, kunatarajiwa kuwanufaisha Wakazi wa Mikoa ya Kagera, Kigoma na Geita.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa wilaya ya Chato Mhadisi Charles Kabeho amesema fedha inayotekeleza ujenzi huo shilingi bilioni Moja zimetolewa na Serikali ya awamu ya tano chini ya Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli kwa lengo la kuboresha huduma za afya katika hospitali hiyo.

Bw. Kabeho amesema ujenzi wa majengo mapya unaendelea na kwamba
mradi huo utakapokamilika utawanufaisha wananchi wa ndani na nje ya
nchi zikiwemo Burundi na Ruwanda.

Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo, Dr. Ligobert Kalisa amesema baada ya ujenzi huo kukamilika utasaidia kuboresha huduma za afya katika kuhudumia wagonjwa wa matibabu ya nje.

Naye Mkuu wa mkoa wa Geita Mhadisi Robert Gabriel amesema serikali inaendelea kuboresha huduma za afya katika hospitali za wilaya mkoani humo kwa lengo la kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi.

Post a Comment

0 Comments