habari Mpya


TRA Ngara yakamata Maziwa ya Magendo Mpakani Rusumo.

Mkuu wa wilaya ya Ngara mkoani Kagera Luten Kanali Michael Mntenjele akizungumza na mwandishi wa Habari wa Radio Kwizera -Kanyesha Faustine  kuhusu maboksi 102 ya Maziwa ya Kampuni ya INYANGE kutoka Rwanda  yaliyokamatwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA wilaya ya Ngara baada ya kuingizwa  nchini kinyume cha taratibu  na wafanyabiashara   kushindwa kulipiwa kodi.
Akizungumza wakati wa kugawa maziwa hayo kwa watu wasiojiweza na mashirika ya kuhudumia watoto wilaya ya Ngara,  Luten Kanali Michael Mntenjele amesema kuwa maziwa hayo yamekamatwa yakiingizwa nchini kinyume cha sheria kwa baadhi ya wafanya bishara kukwepa kulipa kodi.

Amewataka Wafanyabiashara wilayani Ngara mkoani Kagera kutii sharia za uingizaji bidhaa za nje ndani ya nchi,  kwani ni ruksa kuingiza biahaa kutoka nje ya nchi lakini utaratibu wa uingizaji unapaswa ufuatwe ikiwa ni pamoja na ulipaji wa kodi.

Nae Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA wilaya ya Ngara Bw.  Mohamed Omary Kapera amesema kuwa  maziwa hayo yamekamatwa kutoka kwa wafanyabiashara mbalimbali katika mpaka wa rusumo unaotenganisha nchi za Tanzania  na Rwanda.

Post a Comment

0 Comments