habari Mpya


‘’Shikamaneni na Kuungana Kulitangaza neno la Mungu ‘’- Askofu Niwemugizi.

Baba Askofu Severini Niwemugizi akisalimiana na Waamini wa Kanisa Katoliki la Mt. Fransisico wa Asiz lililopo mjini Ngara Jimbo Katoliki Rulenge Ngara.


Wakristo Wilayani Ngara Mkoani Kagera wametakiwa kutogawanyika katika madhehebu yao badala yake washikamane na kuungana kwa pamoja kulitangaza neno la Mungu.

Hayo yameelezwa na Askofu wa jimbo katoliki la Rulenge Ngara Muhashamu Askofu Severini Niwemugizi  January 26,2020 wakati wa Homilia takatifu ya misa ya utoaji wa daraja la ushemasi kwa Shemasi Obadia Tembelea. 

Aidha Askofu Severini amewaagiza mapadre wa jimbo la Rulenge Ngara Kuheshimu na kuthamini mimbali na madhabahu maana ni sehemu pekee inayo tumika kulitangaza neno la Mungu.

Kwa upande wao baadhi ya waumini walio hudhuria ibada hiyo wamempongeza Shemasi Tembelea kwakupata daraja hilo huku wakiamini kuwa atafanya kazi ya kulitangaza neno la Mungu ili watu waweze kuokoka na kutenda yaliyo mema.

Post a Comment

0 Comments