habari Mpya


Serikali mkoani Kagera Yaombwa Kuzihamisha Kaya Kupisha Athari za Maafa ya Mafuriko.

Na Anord Kailembo –RK Bukoba.

Serikali mkoani Kagera imetakiwa kuwahamishia maeneo mengine baadhi ya wananchi wa manispaa ya Bukoba ambao wamekuwa wakikumbana na changamoto ya mafuriko mara kwa mara kipindi cha mvua kutokana na kuishi bondeni.
 Mkuu wa zima moto mkoani Kagera Bw. Hamis Shaaban amesema hayo wakati akizungumza na redio Kwizara na kwamba baadhi ya wananchi wamekuwa wakilazimisha kuishi maeneo hatarishi kwa sababu hawana uwezo wa kipato utakaowawezesha kuanzisha makazi mengine.
Muonekano wa Nyumba zikiwa katikati ya maji katika mtaa wa Omukigusha, wakazi wa nyumba hizo hulazimika kuziama nyumba zao kwa maji kujaa. 
Amesema kuwa ni vyema serikali ifikirie kuwatafutia maeneo maalumu ya kuhamia ili kuepusha gharama inayotumika kuwahudumia pindi yanapokuwa yametokea mafuriko.

Baadhi ya wakazi wa maeneo ya Kanoni manispaa ya Bukoba ambao wamekuwa wakikubwa na mamfuriko wamesema kuwa ufikapo msimu wa mvua hukumbwa na hofu ya kuharibikiwa na mali zao, kuvamiwa na maji huku wakikiri kuwa uduni wa maisha ndicho chanzo cha kutokutoka kwenye maeneo hayo.
Huu ni Mto Kanoni  huwa unafurika  maji kutokana na mafuriko yanayosababishwa na mvua kubwa zikinyesha Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.

Picha na Maktaba yetu.

Post a Comment

0 Comments