habari Mpya


Rais Magufuli Leo January 10 Aanza Ziara ya Kikazi Visiwani Zanzibar.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 09 Januari, 2020 amewasili Jijini Dar es Salaam akitokea nyumbani kwake Chato, Mkoani Geita.
Rais Magufuli ambaye ameongozana na Mkewe Mama Janeth Magufuli leo Ijumaa January 10, 2020 ataanza ziara ya kikazi Visiwani Zanzibar ambako ataweka jiwe la msingi la jengo la Idara ya Usalama wa Taifa Zanzibar.
Keshokutwa (11 Januari, 2020), Rais Magufuli ataweka jiwe la msingi la Shule ya Sekondari ya Mwanakwerekwe iliyopo Mjini Magharibi na atafungua hoteli yenye hadhi ya nyota tano iitwayo Hotel Verde Azam Luxury Resort and Spa iliyopo Mtoni.
Rais Magufuli atashiriki Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 56 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar zitakazofanyika Jumapili tarehe 12 Januari, 2020 katika uwanja wa Amaan, Mjini Magharibi.

Post a Comment

0 Comments