habari Mpya


Mtibwa Sugar Yaisubiri Azam FC au Simba Fainali Kombe la Mapinduzi 2020.

Timu ya Mtibwa Sugar imefanikiwa kwenda hatua ya Fainali ya Kombe la Mapinduzi 2020 kwa kushinda penalti 4-2  baada ya kufungana goli 1-1 ndani ya dakika 90 na Yanga SC  jana January 9, 2020 Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Kipa wa tatu wa Yanga, Ramadhani Kabwili alipangua penalti ya kiungo Abdulhalim Humud ‘Gaucho’, lakini wenzake beki Kelvin Yondani akagongesha mwamba na kiungo Abdulaziz Makame akapiga juu ya lango.

Nusu Fainali ya pili inachezwa leo ijumaa January 10,2020 baina ya Mabingwa wa Tanzania Bara, Simba SC dhidi ya washindi wa Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Azam FC Saa 2:15 usiku kwenye Uwanja wa Amaan. 
Mchezo huo, ulishuhudiwa na kocha Mbelgiji, Luc Aymael aliyewasili Dar es Salaam Alhamis kwa ajili ya kukamilisha mipango ya kujiunga na timu hiyo na moja kwa moja kwenda kuungana na timu Visiwani Zanzibar.

Luc Aymael anakuja Yanga SC baada ya kuzifundisha klabu za AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Missile ya Gabon, AFC Leopard ya Kenya, Rayon Sport ya Rwanda, JS Kairouan ya Tunisia, Al Nasr ya Dubai, Al Merreikh ya Sudan, Polokwane City, Free State Stars, Black Leopard za Afrika Kusini na Tala'ea El Gaish ya Misri.

Post a Comment

0 Comments