habari Mpya


Milioni Zaidi ya 400 Kuboresha Barabara za TARURA Kakonko.

Na Samuel Masunzu –RK Kakonko.

Kiasi cha shilingi milioni 499, laki 2 na elfu 40 zinatarajia kurekebisha miundombinu ya barabara zilizopo chini ya wakala wa barabara za mjini na vijijini TARURA wilayani Kakonko Mkoani Kigoma. 

Mhandisi Erasto Mlengera kutoka ofsi za TARURA wilayani Kibondo amesema mpango huo ni katika kuhakikisha miundombinu ya barabara inaimalika. 

Aidha matengenezo hayo yatahusisha ukarabati wa maeneo mabovu zaidi, pamoja na matengenezo ya muda maalumu ambapo mikataba minne imekwisha kusainiwa na wakandarasi kwa ajili ya shughuli hiyo.
Mikataba hiyo imelegwa kutekelezwa kwa mwaka 2020 ili kuiweka miundombinu ya Barabara katika hali ya kupitika hasa barabara za mitaa zilizopo chini ya TARURA.

Post a Comment

0 Comments