habari Mpya


Mchezaji Kobe Bryant Afariki katika Ajali ya Helikopta.

Nyota wa mpira wa vipaku nchini Marekani Kobe Bryant na binti yake Gianna ni miongoni mwa watu tisa waliofariki katika ajali ya helkopta iliyotokea katika mji wa Calabasas, California.

Bryant amefariki akiwa na miaka 41, alikuwa anasafiri na ndege binafsi aina ya helkopta ambayo ilianguka na kuwaka moto.

Mkuu wa polisi wa LA anasema kuwa hakuna yeyote aliyenusurika katika ajali hiyo.

Ripoti za awali zilisema kuwa kulikuwa na watu watano ndani ya ndege hiyo.

Bryant, ambaye ni bingwa wa NBA mara tano alikuwa anatambuliwa duniani katika historia ya kuwa mmoja wa wachezaji bora wa vikapu.

Salamu za rambirambi kutoka kwa watu maarufu na wachezaji wenzake nyota huyo aliyecheza mpira wa kikapu kwa miaka 20 na kustaafu april 2016, zimekuwa zikimiminika kuonyesha mshtuko wa kifo cha nyota huyo wa mpira wa vikapu.

Mafanikio yake ni kuwa Mchezaji  Bingwa wa NBA 2008 mara mbili mfululizo akiibuka mchezaji bora ,mfungaji bora NBA na Bingwa mara mbili wa mashindano ya Olimpiki.

     

Post a Comment

0 Comments