habari Mpya


Mapato Muleba Yaongezeka.

Na Shafiru Yusuf –RK Muleba.

Mapato ya ndani ya Halimashauri ya Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera yamepanda kutoka bilioni 3.662 hadi kufikia bilioni 4.220 ikiwa ni ongezeko la shilingi milioni 557 sawa na asilimia 15.22.

Afisa Mipango Wilaya ya Muleba Bw. Evart Kagaruki amesema hayo wakati akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani cha kujadili mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha wa 2020/2021 kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya Wilaya ya Muleba.

Bw. Kagaruki amesema kuwa licha ya kuongezeka kwa mapato hayo bado ruzuku ya mishahara imepanda kutoka bilioni 31.95 hadi bilioni 37.602 ambayo ni ongezeko la shilingi bilioni 5.644 sawa na asilimia 17.66.

Kwa upande wao baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya Muleba, wameshauri kutengwa bajeti ya ufuatiliaji wa shughuli za maendeleo kutokana na baadhi ya watendaji wa serikali kushindwa kuwafikia wananchi na kuwahudumia mahitaji mbalimbali ya maendeleo na kusababishwa kukwama kwa baadhi ya shughuli za maendeleo.

Post a Comment

0 Comments