habari Mpya


Maambukizi ya Ugonjwa wa Ukoma Yapungua Tanzania.

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto ,Mhe.Ummy Mwalimu amesema kiwango cha maambukizi mapya ya ugonjwa wa ukoma umepungua kutoka watu 43 kati ya watu milioni  Moja  2014 hadi watu kufikia wagonjwa 26 kati ya watu milioni Moja mwaka 2019.

Amezungumza hayo January 25,2020 jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na wazee ambao ni waathirika wa ugonjwa wa ukoma katika kijiji cha Samaria Kata ya Hombolo bwawani.

Amesema kupungua kwa maambukizi hayo ni kutokana  na juhudi zaa serikali za kuhakikisha  wanapima na kutoa matibabu bure kwa aathirika wa ugonjwa wa huo.

Pia Waziri Ummy amesema maambukizi mapya Ukoma kwa watoto takriban asilimia 41 % ambapo mwaka 2014 kulikuwa na watoto 90  na wamepungua hadi watoto  53 mwaka 2019.

Kwa upande wake mkurugenzi wa progamu  wa elimu vijini (CHEP) Luteni Kanal  Msaafu Daudi Tandila  amesema  Kulingana na Takwimu hizo,na msimamo wa shirika la afya Duniani (WHO) yakuwa Kati ya wagonjwa elfu kumi akipatikana Mgonjwa Mmoja,italeta ripoti ya kuwa hakuna ugonjwa wa ukoma.

Hivyo Wizara ya afya ikusanye taarifa upya kupata Takwimu zinazotolewa na WHO za udhibitisho wa Kutokuwepo kwa ugonjwa huo.

Post a Comment

0 Comments