habari Mpya


Kituo cha Usuluhishi CRC Chalaani Mauaji ya Wanawake nchini Tanzania.

Kituo cha usuluhishi CRC kilichopo jengo la TAMWA Jijini Dar es salaam, kimelaani wimbi la mauaji ya wanawake wanaouwawa na wanaume lililojitokeza hivi karibuni nchini Tanzania.

Taarifa iliyotolewa na kituo hicho cha Usuluhishi imesema kuwa, matukio ya mauaji kwa wanawake hivi sasa yameshika kasi kubwa nchii Tanzania na vyombo vya habari vimekuwa vikitoa taarifa hizo mara kwa mara.

Mratibu wa CRC Bi. Gladness Munuo amesema kuwa, kuna matukio matatu ya mauaji kwa wanawake yaliyojitokeza mikoa ya Mara, Kigoma na Arusha ambapo wanawake wameuawa na wame zao kwa sababu mbalimbali ikiwemo ya wivu wa kimapenzi. 

Amesema matukio ya mauaji haya ni miongoni mwa mengi yaliyojitokeza mwishoni mwa mwaka 2019 na mwanzoni mwa mwaka huu, ambapo baadhi ya wanandoa ama watu wanaoishi pamoja kama mke na mume wameamua kujichukulia sheria mkononi na kukatisha maisha ya wenzao.


Aidha kituo cha CRC imewaomba wananchi kuwa na hofu ya Mungu, pia jeshi la polisi lifuatilie kwa karibu usalama wa raia ili wanaohusika na vitendo hivyo wachukuliwe hatua za kisheria.

Post a Comment

0 Comments