habari Mpya


‘’Historia Imeandikwa’’- Tawi la kwanza Bungeni (Wekundu wa Mjengoni),”

Mabingwa watetezi wa Ligi kuu soka Tanzania Bara, Simba SC Jumatano ya Januari 29/ 2020 imeandika historia mpya kwenye ulimwengu wa soka kwa kuwa klabu  ya kwanza ya soka Tanzania kufungua tawi la Simba Bungeni (Wekundu wa Mjengoni).

 Tawi hilo limezinduliwa na Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akiambatana na Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson ambao wote ni Mashabiki wa Simba.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai akionekana kukata utepe kuashiria kuzinduliwa rasmi kwa tawi hilo lililopewa jina la ‘Wekundu wa Mjengoni’.
Kwa upande wao Simba imeandika kuwa hilo ni tawi la kwanza Bungeni ”HISTORIA IMEANDIKWA. Tawi la kwanza Bungeni (Wekundu wa Mjengoni),” Imeandika Simba SC kupitia akaunti yake ya Instagram.

Simba itakuwa klabu ya kwanza inayoshiriki ligi kuu nchini kuwa na tawi lake Bungeni jijini Dodoma.

Post a Comment

0 Comments